Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dr. Festus Ilako (Kulia) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Naibu Mkurugenzi Dr. Rita Noronha.
Msanii maarufu wa kizazi kipya Banan Zorro ametangazwa pia kuwa balozi wa Kampeni hii ya Stand Up for African Mothers inayoendeshwa na Amref kusomesha wakunga ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Msanii Maarufu wa Kizazi Kipya Mwasiti( Kulia) ametangazwa kama Balozi wa kampeni ya Stand Up For African Mothers, akiongea na waandishi wa habari.
Na Mwandishi Wetu.
Nchini Tanzania, wanawake 7,900 hupoteza maisha kila mwaka wakati wa kujifungua. Zaidi ya asilimia 80 ya vifo hivi vingeweza kuepukika endapo wahudumu wa afya wenye utaalamu wangetoa huduma kwa wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua. Kwa kuamini kuwa hakuna mwanamke anayepaswa kufa wakati wa kujifungua, Shirika la Amref Health Africa Tanzania kwa kushirikiana na Bank za Barclays na Bank M leo wametangaza nia ya kuongeza nguvu na juhudi za kutunisha mfuko wa kusaidia mafunzo ya wakunga kupitia kampeni yake ya Stand up for African Mothers.
Kampeni hiyo ya kimataifa inalenga katika kuongeza uelewa juu ya mchango unaotolewa na wakunga wenye ujuzi katika kupunguza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua na watoto wachanga. Kampeni hii pia inalenga kukusanya fedha kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wakunga 15,000 katika nchi 13 za Afrika, kati yao wakunga 3800 wanatarajiwa kupata mafunzo nchini Tanzania ifikapo mwaka 2015/2016. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Changia mafunzo ya wakunga , okoa maisha ya mama na mtoto” kwa kuunga mkono nia hii njema unasaidia kuwapatia mafunzo wahudumu wa afya walio mstari wa mbele kuokoa maisha ya mama na mtoto nchini Tanzania
Nchini Tanzania kampeni hii ilizinduliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete tarehe 15 Mei mwaka 2012. Mke wa Raisi amekuwa balozi wa kampeni hii akiongoza juhudi za kuwaokoa kina mama wa kiafrika. Tunayo furaha pia ya kuwatangaza wanamuziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Banana Zoro na Mwasiti Almasi ambao wamejitoa katika kushiriki na Amref Health Africa kuelimisha jamii juu ya afya ya mama na mtoto kupitia kampeni hii ya Stand up for African Mothers.
Mpaka sasa, fedha zilichongishwa kupitia kampeni hii zimewezesha kusomesha wakunga 80 kwa kiwango cha cheti; wakunga 10 wanatarajiwa kuhitimu mwezi wa 11 mwaka huu na 70 wanaingia mwaka wa pili wa mafunzo yao. Jumla ya wanafunzi 176 wanaongeza ujuzi kwa kupata mafunzo ya ukunga kwa njia ya masafa, ili kuongeza elimu kutoka kiwango cha cheti hadi diploma. Mafunzo hayo yanaendeshwa kati ka vituo kumi vilivyo katika mikoa ya Mbeya, Dodoma, Tanga, Kilimanjaro, Mwanza, Mara, Zanzibar and Mtwara. Na kiasi cha fedha kilichopatikana mwaka 2013 kinatarajia kusaidia wanafunzi 60 watakaoanza masomo yao mwezi wa 10 mwaka huu.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo Mkurugenzi wa Amref Tanzania Dr. Festus Ilako alisema “Tunatoa mchango wetu katika kulisaidia Taifa kufikia malengo yake ya millennia (MDGs) yanayohusiana na afya kwa kuboresha huduma za afya na kuchangia katika kuboresha hali ya sasa ya afya ya uzazi. Mafunzo ya ukunga yatawaongezea ujuzi wakunga walioko na kufundisha wakunga zaidi ambao baada ya kuhitimu watatoa huduma za afya ya uzazi katika zahanati hivyo kuchangia katika kupunguza vifo vya kina mama vinavyoweza kuzuilika. Tunatoa rai kwenu kuunga mkono na kubadilisha maisha ya kina mama”
Tunawashukuru wadhamini wote walio pamoja nasi katika kufanikisha juhudi hizi. Bank M na Barclays bank wamekuwa mstari wa mbele katika kusaidia mafunzo ya wakunga kuanzia mwaka 2013 mpaka sasa. Pia tunatambua mchango mkubwa uliotolewa na Benki ya Authetic Media Group, BG, Coca Cola Excel Management, FBME, KPMG, NBC, MICHUZI Blog, Mohan’s LTD, Jaffsher foundation LTD, Jamii forums, KCB bank, UCHUMI Supermarket, IPP Media, Push Mobile, , PWC, Pyramid Pharma, Southern Sun Hotel, Songa's, SERENA Hotels, Serengeti Breweries, Stanbic Bank and TCRA.
Ombi letu kwa mashirika, makampuni ya uma na yale ya binafsi, pamoja na watu binafsi ni kuunga mkono jitihada hizi kwa kudhamini mafunzo ya wakunga (mafunzo ya mkunga mmoja yanagharimu dola 3000). Unaweza kuchangia kwa njia mbali mbali, ikiwa ni pamoja na kupitia
• Account ya benki National Bank of Commerce (NBC), Corporate Branch, Akaunti Namba 0111030004548
• Mpesa Namba 0762 22 33 48
• Tigo pesa Namba 0716 032 441
• Airtel money Namba 0685 506306.
Toa Maoni Yako:
0 comments: