Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar es Salaam.

Wito umetolewa kwa waganga wa tiba za asili nchini kufanya shughuli zao kwa kuzingatia maadili ya kazi zao ilikuepuka dhana potofu ya yakwamba wao ni matapeli.

Hayo ameyasema waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif Rashid jijini Dar es Salaam wakati akitoa tamko la maadhimisho ya siku ya tiba asili ya mwafrika.

Dkt Rashid ameeleza kwamba lengo la maadhimisho hayo ni kuwapa changamoto waganga hao katika kupanga mpango mkakati wa kufufua ari mpya na kujijengea heshima kwa wananchi pamoja na kuondoa vitendo vibaya vinanvyochafua taaluma yao.

Aidha Dkt Rashid ametoa fursa kwa waganga hao kushirikiana na wataalamu katika kitengo cha Tiba asilia Muhimbili ilitiba zao ziweze sahihi na zenyeu bora katika jamii.

Hata hivyo ametoa sushauri kwa waganga hao kujiepusha na matangazo yanayokizana na taarifa za kiutafiti katika suala zima la kutibu na kuponya magonjwa mbalimba liikiwemo Ukimwi.

Siku ya Tiba za asili ya mwafrika uadhimishwa kila mwaka Agosti 31 ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu yake ni “USHIRIKIANO KATI YA WATOA HUDUMA NA TIBA ASILIA NA TIBA YA KISASA”
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: