Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglicana Tanzania Jacob Chimeleja, Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi, Mbunge wa Mpwapwa Mheshimiwa Gregory Teu, Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa George Simbachawene pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe,  akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi ujenzi wa Daraja la Mto Gulwe lenye urefu wa mita 170.
 Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete wakwanza kushoto  akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli, Mbunge wa Mpwapwa Mheshimiwa Gregory Teu pamoja na
Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa George Simbachawene, akiweka jiwe la
msingi kama ishara ya kuzindua rasmi ujenzi wa Daraja la Mto Gulwe lenye
urefu wa mita 170 litakalo unganisha kati ya Wilaya ya Mpwapwa na
Kibakwe.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakiwa katika picha ya  pamoja na Mkandarasi,viongozi wa dini na kitaifa mara baada ya Rais kuzindua rasmi ujenzi wa daraja la Gulwe.
 Daraja la Gulwe linalotumika sasa kama linavyoonekana hali iliyopelekea Serikali ya awamu ya nne kupitia Wizara ya Ujenzi kuanza kujenga daraja kubwa na la kisasa la Gulwe litakalokuwa na mita 170 mara baada ya kukamilika kwake.
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati akipita mbele ya Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa Daraja la Gulwe lenye urefu wa Mita 170.
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wapili kutoka kulia akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wakwanza kulia, Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi ERB Profesa Ninatubu Lema watatu kutoka kulia pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale wakifatilia ngoma za asili kabla ya uzinduzi rasmi wa Daraja la Gulwe
 Ujenzi wa Makalvati yatakayosaidia Daraja kupitisha maji katika mto Gulwe kama yanavyoonekana. Jumla ya Makalvati tisa yatajengwa katika daraja hilo la mita 170.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: