Meriam akutana pia na Papa Francis na kubarikiwa yeye na mtoto wake aliyejifungua akiwa jela.

Mwanamke wa Sudan aliyenusurika hukumu ya kifo nchini mwake kutokana na kuukana Uislam amesafirishwa kwa ndege hadi Italia baada ya kukaa kwa zaidi ya mwezi mmoja kwenye ubalozi wa Marekani huko Khartoum.

Meriam Yahia Ibrahim Ishag pamoja na familia yake walipokelewa Roma na Waziri Mkuu wa Italia, Matteo Renzi, ambaye alisema leo ni siku ya kusherehekea.

Baba wa Meriam ni muislam mama mkristo na kwa mujibu wa sheria za Kiislam mwanamke huyo alipaswa kuwa muislam na hakutakiwa kubadili dini na kuwa mkristo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: