Mfalme wa Uholanzi, Willem-Alexander akiwa na Malkia Maxima wakiwa mjini Eindhoven wakisubiri kupokea miili ya abiria waliopoteza maisha yao baada ya ndege ya Malaysia kutunguliwa na waasi wanaoungwa na mkono nchini Ukraine. 
 Msafara wa magari yaliyobeba miili ya abiria 40 kati ya 298 waliofariki dunia katika ajali ya ndege ya Malaysia baada ya kutunguliwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi ukiongozwa na askari waliokuwa katika pikipiki mjini Eindhoven, Uholanzi baada ya kuwasili kutoka Ukraine jana jumatano.
Miili ya abiria 40 kati ya 298 waliopoteza maisha yao katika ndege ya Malaysia iliyotunguliwa na waasi nchini Ukraine, imewasili nchini Uholanzi na kupokelewa na maelfu ya wananchi waliofurika barabarani wakiwa na majonzi kuwapokea wapendwa wao. 

Kati ya abiria hao 298 wakiwemo wahudumu wa ndege hiyo waliopoteza maisha, 193 ni raia wa Uholanzi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: