Kushoto ni Mtuhumiwa Jacob Mayani kinara wa ubakaji, ulawiti na kutoboa macho watoto mkoani Shinyanga akiwa chini ya ulinzi mara baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha.

Na Mwandishi Wetu.

Mtuhumiwa aliyekuwa akikabiliwa na kesi za ubakaji na kulawiti watoto katika Manispaa ya Shinyanga amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kesi tatu tofauti.

Mtuhumiwa huyo Jacob Mayani au maarufu kwa jina la Boy mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa manspaa ya Shinyanga amehukumiwa vifungo vitatu vya maisha kwenye Mahakama ya Hakimu mkazi Mfawidhi Shinyanga.

Jacob Mayani ambaye alituhumiwa kuhusika na  matukio tofauti ya ubakaji na kulawiti watoto chini ya miaka 10 Sanjari na kuwatoboa macho amejikuta akiishia gerezani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: