IMG-20140729-WA0009
Huu ndio ukweli kuhusu picha za Dayna na Nando zilizozua maswali mengi, kama ni mapenzi au kazi!

Hatimaye jibu la maswali yaliyojitokeza zaidi ya mwezi mmoja uliopita baada ya picha za Dayna na Nando wakiwa katika hali iliyoashiria kuna kitu zaidi ya urafiki baina yao, limepatikana.

Ijumaa hii (August 1) Dayna anaachia video ya single yake mpya ‘I DO’ ambayo mshiriki wa Big Brother 2014 Ammy Nando amecheza kama mpenzi wa Dayna katika kichupa hicho.

Video imeandaliwa na Kwetu Studios na audio ambayo tayari imetangulia kutoka imetengenezwa na producer Triss wa Morogoro ambaye kwa sasa amefungua studio iitwayo Conga Music jijini Dar es salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: