Afisa Masoko wa Benki ya Twiga Bancorp Bwa.Adalbert Alchard akizungumza  na Wanahabari nje ya banda lao kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo kwa wateja wao, kwenye maonyesho ya biashara ya Kimataifa ya 38 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwal.Julius Nyerere jijini Dar.Pichani kushoto ni  Afisa wa Benki hiyo,Bi Tuddy Lutengan.
Pichani ni  Meneja wa Tawi lililopo ndani ya  maonyesho ya biashara ya Kimataifa
ya 38 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwal.Julius Nyerere jijini Dar
,Bi. Upendo Tendewa akifafanua zaidi huduma zitolewazo na benki hiyo.Bi.Upendo amesema kuwa dhamira yao kubwa ni kukidhi mahitaji ya wateja ya kibenki na ya kifedha kwa kuhakikisha upatikanaji wa bidha na huduma bora kabisa katika soko  kwa bei inayowezekana kulipa na viwango  vyenye manufaa yanayolingana na gharama na faida ya kurudhisha kwa mwanahisa.

Amesma benki hiyo inatumia kadi yako iitwayo Twiga ExpressCard ambayo mteja anaweza kuitumia kupata huduma za kibenki katika ATM yoyote iliyounganishwa na mtandano wa UMOJA SWITCH,ambapo zaidi ya ATM 180 na mabenki ishirini nna nne nchini yameunganishwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: