NYOTA aliyebeba matumaini ya Wabrazil wengi, Neymar amefunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Croatia kwenye mchezo wa ufunguzi wa fainali za kombe la dunia.

Wenyeji walijifunga mapema dakika ya 7 ya kipindi cha kwanza baada ya Marcelo kuujaza mpira nyavuni katika harakati za kuokoa na kuzua ukimya mkubwa uwanjani kwa mashabiki wa Brazil waliofurika kushuhudia timu yao.

Mambo almanusura yawe mabaya kwa Brazil wakati Neymar alipomfanyia faulo mbaya kiungo wa Croatia Luka Modric, lakini mwamuzi Yuichi Nishimura alimzawadia kadi ya njano tu.

Baadaye Neymar alifunga bao la kusawazisha kwa shuti la mbali na aliongeza bao la pili kwa njia ya mkwaju ya penati baada ya mwamuzi kutoa penati yenye utata kufuatia Dehan Lovren kumfanyia madhambi Fred.

Oscar alihitimisha karamu ya mabao kwa Wabrazil na kutoka na ushindi wa kwanza katika michuano ya mwaka huu inayofanyika katika ardhi yao.

Mkwaju wa penati: Neymar alifunga penati yake ingawa kipa wa Croatia aligusa mpira.
Hapa chini ni viwango vya wachezaji wa timu zote na alama zimetolewa juu ya 10.
Neymar ndiye mchezaji bora wa mechi ya leo kwa kupata alama 8 akifuatiwa na Oscar mwenye alama 7.

Kikosi cha Brazil na viwango vyao: Julio Cesar 6; Dani Alves 5.5, Thiago Silva 6, Luiz 6, Marcelo 5.5, Paulinho 6, Gustavo 7, Hulk 6 (Bernard 68), Oscar 7, Neymar 8, Fred 6.5.
Wachezaji wa akiba: Jefferson, Fernandinho, Dante, Maxwell, Henrique, Ramires, Hernanes, Willian, Jo, Maicon, Victor.

Kikosi cha Croatia na viwango vyao: Pletikosa 6, Srna 6.5, Corluka 7, Lovren 6.5, Vrsaljko 6; Modric 7, Rakitic 7, Perisic 6.5, Kovacic 6 (Brozovic 62), Olic 6, Jelavic 6.
Wachezaji wa akiba: Zelenika, Pranjic, Vukojevic, Schildenfeld, Rebic, Sammir, Vida, Eduardo, Subasic.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: