Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwasili Bungeni alipokuwa anaenda kuwasilisha hotuba ya mapendekezo ya Bajeti ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2014/2015 leo mjini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiingia ukumbi wa Bunge kwa ajili ya Bunge hilo kusomewa hotuba ya Bajeti ya Serikali na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum leo mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akisindikizwa na askari wa Bunge kwenda kusoma Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2014/2015 leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akifungua Mkoba wenye Bajeti ya Serikali ili aanze kuisoma.
Baadhi ya Wabunge wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum alipokuwa anawasilisha mapendekezo ya Bajeti ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2014/2015 leo Bungeni mjini Dodoma.
Baadhi ya Washirika wa Maendeleo nchini wakifuatilia hotuba iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum ya mapendekezo ya Bajeti ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2014/2015 leo Bungeni mjini Dodoma. (Ingiahedi Mduma na E. Mangi - Hazina)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: