Timu ya Mbeya City imetinga Robo Fainali za michuano ya CECAFA Nile Basin Cup inayoendelea nchini Sudan baada ya  sare ya bila kufungana na Enticelles ya Rwanda usiku wa jana katika Uwanja wa Khartoum.

Matokeo hayo yanaifanya timu ya Mbeya City imalize hatua ya makundi kwa kujikusanyia  pointi nne baada ya mechi tatu, lakini ipo katika nafasi ya pili nyuma ya miamba ya soka nchini Kenya, AFC Leopards walioongoza kundi kwa pointi 9.

Mchezo wa mwingine wa usiku, AFC Leopard walishinda bao 1-0 dhidi ya Academie Tchite ya Burundi na kushinda kwa asilimia 100 katika kundi lao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: