Kampuni ya Tigo imeingia katika ushirikiano na mabenki makubwa 17 nchini ili kuwapatia wateja wa tigo pesa uwezo wa kutuma na kupokea pesa kutoka katika akaounti zao za benki kwenda kwenye simu za mikononi.

Mkuu wa huduma za kifedha wa Tigo, Bwana Andrew Hodgson amesema, huduma hii mpya iliyozinduliwa inatarajia kutimiza malengo yetu ya kuwapatia wateja maisha ya kidigitali kwa kupata huduma za kibenki kutoka sehemu yeyote walipo kupitia simu zao za mikononi.

Huduma hii mpya inatarajia kuwapa wateja usalama wa kifedha pamoja na kuepuka kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya kutoa na kuweka pesa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: