Na Mwandishi Wetu

KIKOSI cha Simba, leo kinashuka kwenye uwanja wa Taifa kucheza na Ashanti United kwenye mchezo wa ligi kuu huku wekundu hao wa msimbazi wakisaka heshima kwenye mchezo huo kwa kuwa hawana uhakika wa ubingwa msimu huu.

Kocha msaidizi wa Simba, Suleiman Matola, aliiambia Nipashe Jumapili kuwa wanataka ushindi hili kulinda heshima mbele ya vijana hao wa Ilala.

"Tunataka tumalize vizuri..., ni kweli kwa sasa tunataka kuweka heshima k timu tutakazokabiliana nazo, tumejipanga kuhakikisha tunashinda michezo yote na kwa Ashanti tuna uhakika wa ushindi," alisema Matola.

Aidha, alisema kuwa pamoja na kuwa wamepania ushindi wanafahamu mchezo utakuwa mgumu kwa kuwa wanakutana na mlimu ambaye alikuwa Simba mwanzo mwa msimu huu.

"Mimi binafsi namuheshimu sana Kibadeni, ni kocha mzuri na nategemea upinzani mkub kutoka kwake," aliongezea kusema Matola.

Kwa upande wake, kocha wa Ashanti United, abdallah Kibadeni, alisema kuwa anaifahamu vizuri Simba hivyo anajua nini cha kufanya ili kuibuka na ushindi.

"Kwangu ni mchezo wa kawaida tu..., naifahamu Simba vizuri,lakini tusubiri mpaka dakika 90 ili kumpata mshindi," alisema Kibadeni.

Simba inshuka uwanjani leo huku ikiwa imekata tamaa na ubingwa msimu huu huku pia iki haina uhakika wa kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa yanayoandaliwa na Shirikisho la soka barani Afrika (CAF).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: