Mwili wa marehemu ukipandishwa kwenye gari Tayari kwenda kuzikwa baada ya ibada ya kumuombea.
Msafara ukielekea makaburi ya Mwananyamala kwa kopa.
Mwili wa marehemu ukishushwa kaburini tayari kwa kuzikwa.


Wanamuziki wenzake na marehemu wakifuatilia mazishi ya mwenzao.
Mchungaji akisoma neno

Mchungaji akirusha udongo kuonyesha ishara ya kuaza maziko

Mke wa marehemu akirusha udongo ndani ya kaburini

Watoto wa kiume wa marehemu wakirusha udongo kaburini kumzika baba yao

Kaka wa marehemu akiwa  akimzika mdogo wake

Mkurugenzi wa Skylight Band akirusha udongo kumzika msanii wake
Aneth kushaba akirusha udongo kumzika marehemu

Waombolezaji wakiwa wanafuatilia maziko kwa huzuni kubwa

Mchungaji akiweka msalaba kwenye kaburi la marehemu

Mke wa marehemu akiweka shada la maua kwenye kaburi.
Watoto wa marehemu wakiweka shada la maua kwenye kaburi na Baba yao
Ndugu wa Marehemu wakiweka Shada la maua
Mpiga Gita mahiri wa bendi ya Skylight Chill challa amezikwa jana kwenye makaburi ya Mwananyamala kwa kopa na mamia ya watu na wanamuziki wenzie.Marehemu Chill challa alifariki Tar 17-04-2014 hospitali ya Taifa ya Muhimbili.Chanzo cha kifo cha marehemu ni shinikizo la damu ambapo kabla ya kifo chake alikuwa katika afya njema,lakini Usiku wa Tar 16 marehemu alidondoka gafla bafuni na ndipo alipkimbizwa hospitalini.

Madaktari walijitaidi kwa kila hali na mali kuokoa uhai wa marehemu lakini ilishindikana kutokana na shinikzo la damu kuwa kubwa sana na ndipo Chill challa akafariki dunia,Marehemu Chill challa ameacha Mke na watoto wawili,Marehemu alikuwa ni mpiga gita mzoefu na mahiri ambaye amepitia karibu bendi zote kubwa na kongwe nchini kama Akudo,Fm academia Nk.

Uongozi mzima wa Skylight band unawashukuru wale wote waliojitoa kwenye msiba huu na Mungu awabariki. PICHA ZOTE NA DJ SEK BLOG
Baadhi ya waombolezaji wakibadilishana mawazo Katikati ni Mwanamuziki wa Skylight band Joniko Flower

Waombolezaji wakiendelea kubadilishana mawazo wakati wakisubili mwili wa marehemu Kufika,Mwenye Baibui nyeusi ni mke wa Chicago Matelephone na wanamuziki wa Skylight band

Mkurugenzi wa Skylight Band akijadili jambo na Aneth Kushaba ili kuweka mambo sawa kabla ya Mwili wa marehemu kuwasili.

Gari iliyobeba Mwili wa marehemu Chill Challa likiwasili Nyumbani kwa marehemu
Ndugu na Jamaa wakishusha Mwili wa marehemu Chili Challa

Mwili wa Marehemu ukishushwa kwa ajili ya ibada.
Mchungaji wa kanisa alipokuwa Anasali marehemu akiongoza ibada ya kumuombea Marehemu Ayoub Songoro maaru Chill challa aliyekuwa mwanamuziki na mpiga Gita wa Skylight Band.

Misa ya kumuombea Marehemu akiendelea Nyumbani kwake Mwananyamala.
Mke wa marehemu akiwa na majonzi.
Meneja wa bendi Ya Skylight Aneth Kushaba akiaga mwili wa marehemu
Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu
Mkurugenzi wa Skylight Band akiaga Mwili wa marehemu
Watoto wa marehemu wakiwa na majonzi ya kuondokewa na baba yao kipenzi
Kaka wa marehemu akiaga mwili wa mdogo wake kwa huzuni kubwa
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: