Baba mmoja ambaye ni mwanandoa jana alizua balaa kwa mkewe baada ya kumpigia simu na mazungumzo yao yalianza hiv; halloo mke wangu.., yaani ni shidaa sitaweza kurudi nyumbani daraja limevunjika na kutoka Morogoro kurudi Dar haiwezekani. 

MAMA: Mme wangu morogoro ulienda bila kuniaga! ?

BABA: Ilikuwa ni ghafla sana mke wangu sikuweza kukwambia

MAMA: Kha! Sasa watoto nani atawaangalia

BABA: Unasemaje! We uko wapi kwani

MAMA: Niko bagamoyo na daraja limeondolewa na maji sitaweza kurudi.

BABA: Unasemaje we mwanamke.. nakwambia nikukute nyumbani ndani ya dk 15
Baada ya dk 15 Baba kafika nyumbani.

MAMA: Haya umefikaje kutoka Morogoro.

BABA: Nilipewa lifti na Helikopta ya Rais JK nilikuwa na Makamu Dkt. Bilal 

MAMA: Wewe mwanaume si helikopta aliyokuwemo makamu wa rais imepata ajali kabla ya kuruka uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es salaam.

BABA: Mimi ni majeruhi mmojawapo...

Hahahahaaaaaa uongo mwingine bwana ...
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: