Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Mussa Iombe, sehemu ya Daraja la Mpiji linalounganisha Bagamoyo na Dar es Salaam, lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini, wakati Makamu alipofanya ziara hiyo ya kujionea maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo leo Aprili 13, 2014. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wanaosimamia shughuli ya daraja hilo, baada ya kuwasili eneo hilo leo. 
Sehemu ya daraja hilo, linavyoonekana baada ya kuongezeka upana kwa kulika kutoka mita 25 na sasa kufikia mita 75, ambapo tayari Malori yameanza kumwaga vifusi vya mawe ili kuziba eneo hilo na kuweza kuunganisha njia hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi kuelekea eneo la tukio kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika kutokana na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini. Picha na OMR
Nguzo za umeme zikiwa zimeinama baada ya kuzidiwa nguvu na maji hayo yaliyobomoa daraja. 
Malori yakimwaga vifusi vya Mawe kwenye daraja hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Mussa Ibrahim Iombe, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhitimisha ziara yake hiyo, katika eneo la Daraja la Mpiji, linalounganisha Bagamoyo na Dar es Salaam, leo Aprili 13, 2014. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka eneo la tukio Daraja la Mpiji baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: