Na Mwandishi Wetu

Vinara wa Ligi Kuu Bara Azam FC, wameanza kujipanga tayari kwa msimu ujao baada ya kumsainisha mshambuliaji Ismailla Diarra mkataba wa miaka miwili.

Uamuzi huo unakuja kufuatia majaribio ya wiki mbili aliyoyafanya Diarra katika timu hiyo, akisimamiwa na kocha wa timu hiyo Joseph Omog raia wa Cameroon.

Taarifa ambazo zimefikia dawati letu kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo, umesema Diara aliyekuwa akiitumikia timu ya Bamako de Olyimpic inayoshiriki ligi kuu nchini humo, tayari ameshasainishwa mkataba wa miaka miwili kuitumikia Azam ambao wapo karibu kutangazwa mabingwa wapya wa ligi ya bara.

Kusajiliwa kwa Diarra kuna kuwa ni kukamilisha idadi ya nyota watano wa kimataifa wanaohitajika na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambapo sasa watakuwa na Kipre Tchetche, Kipre Balou, Brian Umony ambaye inaelezwa anaweza kuachwa kumpisha Mganda mwenzake Owen Kasule.

Akithibitisha hilo Katibu Mkuu wa Azam FC Nasoro Idrissa alisema tayari Azam imeshamalizana na mshambuliaji huyo ambapo sasa wanauhakika wa kuwa naye katika msimu ujao baada ya uwezo wake kumvutia Omog.

"Ninachoweza kusema ni kwamba Diarra sasa ni mchezaji wetu na tutakuwa naye katika kikosi chetu katika msimu ujao wa ligi na mashindano mengine tutakayoshiriki,amefanya majaribio na kifupi ni kwamba uwezo wake umekubaliwa na kocha wetu (Omog)", alisema Idrissa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: