Meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini Brighton Majwala akimkabidhi vitabu vya sayansi kwa mkuu wa wilaya Arusha John Mongela kwa ajili ya shule ya sekondari Naura ya jijini Arusha vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya airtel chini ya mpango wake wa Shule Yetu.
Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela akimkabidhi vitabu mbalimbali mkuu wa shule ya sekondari Naura Sunday Mushobozi vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania katika hafla iliyofanyika shuleni hapo.
---
Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela aliwashukuru Airtel kwa msaada wa vitabu kwa shule ya sekondari ya Naura na kusema kuwa licha ya kuwa ni jukumu la Serikali kutoa vitabu kwa shule lakini imekuwa ikizidiwa na majukumu mengi hivyo kwa msaada huo Airtel wanapaswa kupongezwa kwa kutimiza wajibu wao kwa jamii.

Kauli hiyo imetolewa wakati Airtel ilipotoa msaada wa vitabu kwa Shule ya sekondari ya Naura mkoani Arusha chini ya mpango wake maalumu wa “shule yetu” ambapo Mkuu wa wilaya ya Arusha Bwana John Mongela alikuwa mgeni rasmi.

Bwana Mongela alisema “Vitabu ndio nyenzo ya msingi ya kupata maarifa hivyo kwa Airtel kujikita katika kusaidia jamii kupitia vitabu kwa shule za sekondari kutawawezesha wanafunzi na jamii kupata hazina kubwa ya maarifa na mbinu za kujikwamua kiuchumi kupitia vitabu hivi. Napongeza sana jitihada hizi na mpango huu ambao ni endelevu na yenye kugusa shule nyingi na jamii kubwa ya watanzania kwa ujumla”.

Meneja biashar
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: