Mkurugenzi Mtendaji wa Nafasi Art Space Bw. Jan Van Esch akiwa pamoja na Bw. Paul Ndunguru ambaye ni mwanachama wa kituo hicho cha Nafasi Art Space wakiongelea uzinduzi wa programu yao ‘Kujenga weledi wa sanaa na sanaa za maonyesho Tanzania’.
Picha hii imechorwa na Bw. Chitanda ambayo inapatikana kwenye kituo hicho.
Maonyesho ya sanaa ya Lute Mwakisopile ndani ya Nafasi Art Space jijini Dar es Salaam.

 Muimbaji Samuel Hokororo akiimba wimbo katika mkutano na waandishi w habari leo jijini Dar es Salaam ndani ya Nafasi Art Space.
---
Nafasi Art Space inazindua programu ya 'Kujenga weledi wa sanaa na sanaa za maonyesho Tanzania’. Lengo kuu la programu hi ni kujenga jukwaa la kuwawezesha wasanii kufanya kazi, kujifunza na kufanya maonyesho ya sanaa. 

Kwa kutumia programu hii, wasanii watapata fursa na nafasi ya kuendesha shughuli zao za kisanii, kubadilishana mawazo, elimu na mbinu mbalimbali za kisanii, kuongeza na kuimarisha elimu ya mbinu za biashara na jinsi ya kuzalisha kazi zenye ubora zaidi kwaajili ya mauzo. 

Ndani ya miaka kadhaa ijayo, Nafasi imepanga kupanua idadi ya studio za wasanii katika eneo lao kutoka 11 hadi 30 na hivyo, kutoa nafasi za kufanyia kazi kwa hadi wasanii 50.

Siku ya uzinduzi itaanza na matembezi ya kisanii (art parade) kutoka Mwenge saa 9.30 mchana na kuishia kwenye viwanja vya Nafasi Art Space saa 10.30 jioni ambapo kutakuwa na maonyesho, wasanii ndani ya studio, mafunzo ya sanaa mbali mbali, muziki na dansi. Saa 11.30 jioni kutakuwa na na risala kutoka kwa Mwenyekiti, Mabalozi na wawakilishi wa Balozi za Umoja wa Jumuiya ya nchi za Ulaya (EU) , Ubalozi wa Denmark, na wafadhili wakuu wawili wa Nafasi. 

Hii itafuatiwa na uzinduzi rasmi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya habari, utamaduni, vijana na michezo Bi. Sihaba Nkinga. Kutakuwa na uwakilishi kutoka kwa wafadhili wengine wa Nafasi ikiwemo HIVOS, The African Arts Trust (TAAT), CKU, na Vipaji Foundation. Pia tutakaribisha wafadhili wetu wa hisani APM vituo, Uhuru One, Goldstar, na Toyota Tanzania. 

Baada ya uzinduzi rasmi, kuanzia saa 12.30 jioni kutakuwa na maonyesho kutoka kwa Jukwaa la watoto wa mitaani MAKINI, Baba Watoto , DDI , Hoko Roro na bendi ya Wahapahapa. Nafasi Art Space inaendesha programu hii ikishirikiana na Kuona Trust Kituo cha Visual Arts (Kenya), Fabrikken kwa ajili ya Sanaa na Design (Denmark) , na Mawazo ya kisasa Art Centre (Tanzania).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: