Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (mwenye suti nyeusi)
akioneshwa moja ya mashine zilizokuwa zinatumika kutengenezea matairi
katika kiwanda cha General Tyre kilichopo katika jiji la Arusha na
Mwangalizi wa Kiwanda hich, Bw. Leonald Mgoyo. Serikali ina mpango wa
kukifufua kiwanda hicho baada ya kusimama uzalishaji tangu mwaka 2007.
Timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho wakifurahia jambo wakati wa ukaguzi huo.
Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (mwenye suti nyusi)
akiagana na Mwangalizi wa Kiwanda hicho, Bw Leonald Mgoyo baada ya
ukaguzi wa kiwanda hicho. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Maendeleo la Taifa (NDC) Bw. Gideon Nasari na kushoto kwake ni Naibu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Uzalishaji, Bw
Maduka Kessy.
Timu ya wakaguzi wa miradi wa maendeleo wakiangalia mitambo ya kiwanda cha matairi cha General Tyre jijini Arusha.
Picha na Joyce Mkinga,
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO.


Toa Maoni Yako:
0 comments: