“Mabadiliko katika mfumo wa Serikali katika utendaji kazi kupata mafanikio haraka"


Ofisi ya Rais - Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (OR- UUM) imetoa taarifa kwa umma kuwa utekelezaji wa mfumo wa – Big Results Now ! (BRN) unaendelea vizuri. Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) unaweka utaratibu thabiti wa kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa miradi katika maeneo sita ya kimkakati kitaifa (Kilimo, Elimu, Maji, Nishati , Uchukuzi na Utafutaji wa Rasilimali). Mfumo wa BRN unaweka wazi malengo pamoja na kuainisha uwajibikaji kwa kila mshiriki mmoja au taasisi katika utekelezaji wa miradi ya Serikali ili kupata mafanikio haraka.

Kila Wizara inayotekeleza mfumo huu imeanzisha Kitengo cha Kusimamia Utekelezaji (Ministerial Delivery Unit (MDU)) ambacho kinafanya kazi kwa karibu sana na OR-UUM. Majukumu ya MDU ni kufuatilia na kuthamini utekelezaji wa miradi wa kila siku na kuanda taarifa za utekelezaji za kila wiki na mwezi ambazo huwasilishwa OR-UUM. Taarifa za MDU zinajadiliwa kila mwezi kwenye mikutano ya Kamati ya Wizara ya Kusimamia eneo la kimkakati Kitaifa (Steering Committee Meetings) ambayo Mwenyekiti ni Waziri wa Wizara husika pamoja na Baraza la Mageuzi na Ufuatiliaji Utekelezaji ambalo Mwenyekiti ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mikutano hii inalenga kutatua changamoto au vikwazo vilivyojitokeza.

Aidha, Serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha Vitengo vya Kusimamia Utekelezaji katika ngazi za Mikoa (Regional Delivery Units - RDUs) pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Council Delivery Units - CDUs) ili kuongeza ufanisi wa kutekeleza miradi katika ngazi zote.

Bwana Omari Issa, Mtendaji Mkuu wa OR- UUM alisema, “Tanzania ina mawazo makubwa na Dira na mipango sahihi ya kuleta maendeleo. kinachokosekana ni mfumo sahihi wa kufuatilia utekelezaji ili kupata matokeo yaliyolengwa. BRN inaondoa dosari hii. Aidha, BRN inaleta mageuzi ya uwajibikaji katika ngazi zote za utumishi wa umma.

Ili kufanikisha BRN, tunahitaji kupata ushirikiano kutoka sekta binafsi ambayo italeta teknolojia, utaalum wa menejimenti na mtaji. Ili kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi, BRN imeanza mchakato wa kurazinisha mfumo na taratibu za ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) ili tuhakikishe kwamba sekta binfasi inatoa mchango wake stahiki katika kutekeleza BRN
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: