Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikata utepe kufungua rasmi ofisi ya IECO ukanda wa Afrika, yenye makao yake makuu Beijing China iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam Tanzania, leo Feb 5, 2014 kwa ajili ya kuwakilisha nchi za Afrika na tayari imeanza mchakato katika kukabiliana na magugu maji katika Ziwa Viktoria sambamba na shughuli nyingine zinazolenga utunzaji mazingira na namna ya kukabiliana na majanga yanayotokana na athari za tabia nchi. Kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Sola Pawa ndogo maalum kwa kuchajia simu na kusomea baada ya kufungua rasmi ofisi ya IECO ukanda wa Afrika, yenye makao yake makuu Beijing China iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam Tanzania, leo Feb 5, 2014 kwa ajili ya kuwakilisha nchi za Afrika. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akikabidhiwa Nembo ya Taasisi hiyo iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR
Makamu wa Rais Dkt Bilal akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi na viongozi wa ofisi hiyo baada ya kufunguliwa rasmi, eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akiagana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, baara ya uzinduzi huo. Picha na OMR

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: