Afisa Habari kutoka Kitengo cha Habari Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari katika hoteli ya Holiday Inn juu ya changamoto na mafanikio ya mkutano wa mwisho wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 19) na msimamo wa Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla juu ya masuala ya Tabianchi na Mazingira duniani. Kutoka kulia ni Mtaalamu wa mambo ya Nishati na Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Abbas Kitogo, Mwakilishi kutoka Youth of United Nations Association (YUNA) Adam Anthony na mgeni rasmi Naibu Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi.
Naibu Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkutano wa mabadiliko ya Tabianchi (COP 19) amesema kuna ugumu na umuhimu wa mkutano wa mabadiliko ya Tabianchi, na kuongeza kuwa wamekubaliana wawe na mkataba kwa nchi wanachama jinsi ya kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa kwa kiwango ambacho hakitaongeza Madini Joto duniani
Muyungi alisisitiza kwamba kuna umuhimu wa wanachama kukubaliana kwa maandishi na kuandika mkataba vile vile amesema walikubaliana kutokufuta mkataba mama wa 1992, na umuhimu wa kupunguza Gesi Joto na kuangalia uchangiaji wa tatizo la Madini Joto katika duniani.
Mtaalamu wa mambo ya Nishati na Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Abbas Kitogo, akizungumzia masuala ya mipango ya serikali kuhusu mabadiliko ya Tabianchi kupewa kipaumbele katika mipango ya serikali kwa maendeleo ya Taifa kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, alisisitiza kwamba UNDP ina nafasi ya kusaidia kuleta maendeleo kwa Taifa kwa kuweka mipango ya maendeleo yenye kuendana na mabadiliko ya Tabianchi.
Mwakilishi kutoka Youth of United Nations Association (YUNA) Adam Anthony akizungumzia juu ya umuhimu wa kuwashirikisha vijana katika masuala ya Tabianchi na amesema waliafikiana kutengeneza (Task Force Team) ambayo itakuwa na kazi ya kufuatilia mapendekezo na maadhimisho ya mkutano kwa maslahi mapana ya duniani inayowakilisha vijana, vile vile kupata nafasi ya kukaa na vijana wa nchi zingine juu ya matatizo yanayotokana na mabadiliko ya Tabianchi kwenye mazingira, Kilimo na Sekta za Utalii na uhifadhi na Nishati na umuhimu wa vijana kushiriki kikamilifu katika masuala ya kuelimishana mambo ya Tabianchi.
Bw. Anthony amefafanua kuwa baada ya mkutano wa COP 19 uliofanyika Warsaw Poland, hivi karibuni kujipanga kwa vijana na vyombo vya habari katika na mkutano unaokuja wa 2015 wa mabadiliko ya Tabianchi.
Fazal Issa kutoka Mtandao wa Asasi Zisizo za Kiserikali zinazofanya shughuli zake katika Masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi akizungumza kwa undani matokeo ya mabadiliko ya Tabianchi kwa nchi masikini na jinsi zinavyoweza kurudisha nyuma maendelo ya sehemu husika.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa kufafanua yaliojiri katika mkutano wa Warsaw, Poland wa Mabadiliko ya Tabianchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: