Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiweka jiwe la msingi la Benki ya Azania Tawi la Lamadi huku akishuhudiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Azania Bwana William Erio (wa pili kushoto). 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Azania Bwana William Erio(kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Bwana Charles Singili (kulia) wakifurahia hatua ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa uzinduzi wa Benki ya Azania Tawi la Lamadi jana. 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Azania Bwana William Erio(wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Bwana Charles Singili(kushoto) wakikata utepe kuzindua rasmi Benki ya Azania Tawi la Lamadi jana. Kulia nia mkuu wa Mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi walio ndani ya Benki kuhakikisha kuwa huduma inatolewa kwa kuwango. 
Awali mara tu baada ya kuwasilia katika eneo la tukio Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, alisalimiana na wadau wa Benki ya Azania Tawi la Lamadi na mmoja baada ya mwingine huku akitambulishwa.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na Mkurugenzi wa hifadhi ya jamii wa PPF Kanda ya Ziwa Meshark Bandawe ambapo ni moja kati ya wawekezaji ndani ya benki hiyo. 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, akiendelea kusalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Azania Tawi la Lamadi ambapo amewahimiza kufanya kazi kwa bidii ili wananchi wa eneo hilo waone manufaa ya ujio wa benki hiyo katika himaya yao. 
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akihutubia wananchi wa wafanyakazi wa Benki ya Azania tawi la Lamadi ambapo katika kipindi cha miaka 6 benki hiyo imeongeza matawi kumi na mbili na hivyo kuwa na mtandao wa matawi 15 kwa ujumla. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia amewataka wananchi wa Lamadi mkoani Simiyu kujinufaisha kwa kuzichangamkia fursa za uwekezaji zilizomo ndani ya Benki ya Azania kama zifanyavyo taasisi nyingine kubwa za kitanzania. 
Benki ya Azania Tawi la Lamadi mkoani Simiyu, ilipata fursa ya kumtunukia zawadi Rais Jk.
Rais Jakaya Mrisho kikwete akipata picha ya pamoja na Mawaziri wake, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Viongozi wa Benki ya Azania Tawi la Lamadi mara baada ya shughuli ya uzinduzi kukamilika.
Picha ya Rais Jk na wafanyakazi wa Benki ya Azania Tawi la Lamadi.
Sehemu ya wananchi Eneo  la tukio nje ya jengo la Benki ya Azania Tawi la Lamadi.
Kwa sasa wawekezaji wakubwa katika benki hii ni Taasisi za Kitanzania ambazo ni pamoja na mifuko minne ya hifadhi ya jamii ya NSSF, PPF, PSPF na LAPF. 
Jengo la Benk ya Azania lililofunguliwa na Rais Dkt. Jakaya Kikwete Mkoa Simiyu jana
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: