HEINEKEN imetangaza rasmi leo kuendelea kuidhamini ligi ya mabingwa barani ulaya – UEFA. Kwa makubaliano haya, bidhaa hii ya bia ya kimataifa inayoongoza duniani ya Heineken itaendelea kuwa mdhamini mkuu wa mashindano haya ya mpira wa miguu yanayopendwa duniani kotempaka 2018 (pamoja na msimu wa 2017 / 2018).
Heineken imekuwa mdhamini mkuu wa ligi ya mabingwa barani ulaya toka mwaka 2005. Udhamini huu umeiwezesha bia ya Heineken kuweza kukuza hadhi yake hadi kufikia kuwa bia inayopendwa zaidi duniani. Kwa mwaka uliopita mashabiki wa ligi ya UEFA waliokuwa wakifuatilia michuano hii kupitia TV waliongezeka hadi kufikia zaidi ya bilioni nne katika nchi 220 na miji yake wakati huohuo Heineken ikiendelea kukua na kufahamika zaidi.
Kuongeza mkataba wa udhamini kwa ligi hii kunaipa nafasi bia ya Heineken kuwa na haki za kipekee katika mambo mbalimbali yanayoendelea katika ligi hii ikiwa ni pamoja na kutembelea sehemu mbalimbali za viwanja husika za Kombe la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ambavyo vyote hivyo vitaonekana kupitia mitandao ya kijamiizinazomilikiwa na Heineken pamoja na haki ya kuwa muwakilishi rasmi wa ligi ya mabingwa barani ulaya katika video kupitia tovuti: www.uefa.com.
Mpango huu umeijengeaHeineken msingi mzuri wa kuunda kampeni za kisasa na zenye manufaa kwa mtumiaji wa bidhaa hii. Heineken pia imeboresha na kutanua wigo wa matangazo yake hadi Ujerumani, pamoja na hayo imeweza kupata haki maalum za kutangaza katika viwanja kwa teknolojia ya LED na pia haki ya kutangaza katika sehemu mbalimbali muhimu kibiashara.
Ligi ya mabingwa barani ulaya ni kipengele muhimu katika mipango na mikakati ya ukuaji wa bidhaa ya Heineken. Ikiwa ni sehemu ya kampeni inayoendelea ya ‘kuelekea fainali’Heineken imeshatangaza tarehe na maeneo ambapo kombe la ligi ya UEFA litapitishwa chini ya udhamini wake.
Matembezi ya kombe hili kwa mwaka 2014 yatakuwa ni matembezi ya nane mfululizo yanayodhaminiwa na kuwakilishwa na Heineken ambayo yatajumuisha mabara ya marekani kusini, Afrika, and Asia ili kuwapa mashabiki duniani kote nafasi ya kuliona kombe la ligi ya mabingwa barani ulaya kwa ukaribu zaidi, kukutana na wachezaji maarufu na kuona baadhi ya video za mechi zilipokuwa zikishindana kuwania kombe hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: