Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa taasisi ya Global Education Link, AbdulMalki Molel akitoa maelezo jinsi mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ambapo jna ilikuwa ndiyo uzinduzi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika Tanzania, Ammish OWUSU-AMOAH akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mmoja ya wazazi waliohudumiwa na taasisi ya Global Education Link wakitoa ushuhuda wao jinsi watoto wao walivyowezeshwa kutafutiwa nafasi za masomo kwa vyuo vya nje ya nchi bila usumbufu kwa vyuo vinavyotambuliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania. Ambapo wazazi hao walitoa rai yao kwa wazazi wengine kuendelea kuiunga mkono GEL ili isonge mbele zaidi kwa vile inafanya kazi zake kiuhakika bila ya kudanganya.
Waliongeza kuwa kwa sasa wanafunzi wengi wamekuwa na moyo wa kusoma nje ila kuna baadhi ya makampuni ambayo yamekuwa yakiwadanganya na kujikuta wakidondokea kwenye vyuo ambavyo havitambuliki mwisho wake kuishia kupoteza hela na muda. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaama.
Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Magishi Nkwabi Mgasa akiwapongeza kampuni ya Global Education Link kwa kushirikiana na Benki ya Afrika (BOA) kwa kuweza kubuni njia itakayowawezesha wanafunzi wengi waliokuwa wanapenda kwenye kusoma nje ya nchi ila wanakosa pesa. Vile vile aliwaomba wanafunzi kuacha kukurupukia vyuo vya nje bila kutambua kama vinatambulika Tanzania ama lah ili kuwaepushia usumbufu.  Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Naibu katibu mkuu Tamisemi, Zuberi Samataba akiongea machache katika uzinduzi wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi (katikati) akizindua. Pembeni toka kulia ni Wafanyakazi wa GEL, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika Tanzania, Ammish OWUSU-AMOA, Kaimu Katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Magishi Nkwabi Mgasa pamoja na Naibu katibu mkuu Tamisemi, Zuberi Samataba.
Hiki ndicho kilichozinduliwa.
Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi (katikati) akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika Tanzania, Ammish OWUSU-AMOA mara kwa kufanikisha mpango wa utoaji mikopo kwa kushirikiana na GEL. Pembeni ni Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa taasisi ya Global Education Link AbdulMalki Molel, mfanyakazi wa GEL naKaimu Katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania.
Pongezi zikimiminika...
Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi (katikati) akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa taasisi ya Global Education Link AbdulMalki Molel kwa kufanikisha mpango huko wa utoaji mikopo. Katikati ni mfanyakazi wa BOA benki.
Wageni waalikwa wamekifuatilia uzinduzi huo.
Wageni wakiwa makini kabisa.
 Kila mmoja alikuwa makini kufuatilia uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi (kushoto) akifuatilia uzinduzi pamoja na Naibu katibu mkuu Tamisemi, Zuberi Samataba.
---
Na Mwandishi Wetu.

SERIKALI imeziomba taasisi mbalimbali za kifedha zikiwemo benki kuwasaidia watanzania wenye malengo ya kujiunga na elimu ya juu kwa kuweka utaratibu wa kuwakopesha fedha zitakazowasaidia kumudu gharama za masomo vyuoni na hivyo kuinua kiwango cha elimu nchini.

Rai hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam juzi na Mkurugenzi wa elimu ya juu Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi Prof. Sylvia Temu alipokuwa akizindua mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu juu wenye malengo ya kwenda kusoma nje ya nchi ulioanzishwa na taasisi inayojishughulisha na uwakala wa wanafunzi wanaokwenda kusoma nje ya nchi ya Global Education Link (GEL) ikishirikiana na Benki ya Afrika (BOA).

Prof.Temu mbali na kuusifu mpango huo kwa kudai kuwa utaisaidia Serikali katika suala zima la kuwasaidia wanafunzi wenye malengo ya kujiunga na elimu ya juu, alisema anaamini taasisi nyingi za fedha zilizopo nchini zina uwezo wa kumaliza tatizo la wanafunzi kujiunga na elimu ya juu kwa
kuwakopesha.

“Wazo na kuanzisha mpango hili ni zuri na tuna imani kuwa mlifikiria kumsaidia mwananchi kukabiliana na gharama mbalimbali za masomo, ombi langu ni kwa taasisi zingine kujitokeza na kuunga mkono utaratibu huu kwa kuwa utawasaidia wanafunzi wengi kupata elimu” alisema Prof. Temu.

Pamoja na hivyo pia alisema ni vyema taasisi hizo zikaliangalia suala la viwango vya riba inavyoviweka ili kutomkomoa mwananchi jambo ambalo pia linaweza kusaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wanaotaka kujiunga na elimu hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link(GEL) Abdumalik
Mollel alisema kiasi cha Sh Bilioni 40 zimetangwa katika awamu ya kwanza kwa ajili ya kufanikisha mpango huo unaotarajiwa kuwanufahisha wanafunzi 3000.

Alisema kuanzishwa kwa utaratibu huo umelenga kuwasaidia wanafunzi wenye malengo ya kutimiza ndoto yao kwa kujiunga na elimu ya juu lakini wanashindwa kujiunga kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali ukiwemo utaratibu wa ulipaji wa ada unaofanywa na vyuo vingi vya nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Mollel, vyuo vingi hususani vya nje ya nchi vinawataka wanafunzi kulipa ada ya Mwaka mzima sababu aliyosema imekuwa ikiwafanya wanafunzi wengi kushindwa kuimudu kutokana na uwezo mdogo wa wazazi wao na kwamba kupitia mpango huo watakopeshwa fedha hizo ili waweze kutimiza malengo yao.

Naye Mkurugenzi wa Benki ya BOA Ammish Amoah, alisema ubia wa benki hiyo na taasisi ya GEL umelenga kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwapatia wananchi wake elimu.

Alisema pamoja na suala hilo pia BOA ina utaratibu maalumu wa kuwakopesha wanafunzi wenye malengo ya kujiendeleza na kusisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa .
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: