Kupomomoka kwa jengo la ghorofa tatu ndani ya Westgate Mall baada ya mlipuko uliosababisha vifo vya magaidi wa 5 na na wengine 11 kushikiliwa na Polisi siku ya Jumamtatu Sept 23, 2013 kama unavyoonekana katika picha magari yaliyokua yameegeshwa juu ya paa la magesho ya magari yakiwa yameanguka chini kwa mlipuko huo. 


mlipuko uliosababisha jengo la ghorofa 3 kuporomoka baada ya magaidi wa Al Shabab kuvamia Mall hiyo siku ya Jumamosi Sept 21, 2013 na kusababisha vifo nya watu 69 na wengine 175 kujeruhiwa huku kikundi hicho cha Kigaidi kudai kwamba hawataishia hapo mpaka Kenya itakapoondoa majeshi yake Somalia.




Picha za nje ya jengo la Westgate hazioneshi uhalisia wa hali iliyoko ndani ya jengo baada ya shambulio la kigaidi Jumamosi iliyopita jijini Nairobi, Kenya 

Picha hizi zinatoa picha halisi ya jinsi jengo hilo lilivyoharibika vibaya kwa ndani baada ya ghorofa tatu za jengo hilo kudondoka baada ya kupigwa mabomu katika mchakato wa kukabiliana na magaidi. 

Picha hizi pia zinaonesha jinsi magari yaliokuwepo eneo la maegesho ya magari katika jengo hilo yakiwa yameharibiwa kiasi kwamba kuna mengine ambayo huenda hata wamiliki wanaweza kushindwa kuyatambua.



Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: