MNAMO TAREHE 08.10.2013 MAJIRA YA SAA 16:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA RELINI – MLOWO BARABARA YA MLOWO/KAMSAMBA WILAYA YA MBOZIMKOA WA MBEYA. GARI T.353 APR AINA YA TOYOTA HILUX P/UP LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA KISHA KUSABABISHA KIFO CHA MTOTO PETRO S/O KAUNDA, MIAKA 3, KYUSA, PIA MAJERUHI KWA MAMA MZAZI WA MTOTO HUYO AITWAE FAUSTA D/O MBUBA, MIAKA 35, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ITEMPULA AMBAYE AMELAZWA ZAHANATI YA NAZARETH – MLOWO. CHANZO KINACHUNGUZWA.
DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA ZAHANATI HIYO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.

WILAYA YA KYELA – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 08.10.2013 MAJIRA YA SAA 16:00HRS HUKO ENEO LA MBUGANI WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA FRANK S/O ARON, MIAKA 27, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MBUGANI AKIWA NA BHANGI MISOKOTO 20 SAWA NA UZITO WA GRAM 120.
MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Toa Maoni Yako:
0 comments: