Naibu Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo Amos
Makala akizungumza na wakazi wa manispaa ya Iringa wakati wa ufunguzi
rasmi wa Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani
Iringa. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma na
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana kutoka Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Kajugusi akitoa ufafanuzi kuhusu
Maonyesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika kila mwaka nchini wakati wa
Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha Mbio za
Mwenge wa Uhuru na kuwataka vijana kutumia fursa za kiuchumi zilizopo
kujiletea maendeleo.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Amosi Makala akiwa ameambatana na mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt. Christine
Ishengoma wakiangalia banda la Maonyesho la vijana wajasiriamali kutoka
Zanzibar wanaoshiriki Maonyesho ya Wiki ya Vijana mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos
Makala akiangalia gari lililotengenezwa kwa kutumia mbao na vifaa vya
asili na mbunifu Keny Joseph kutoka kijiji cha Nyororo, Mufindi. Gari
hilo ambalo limekua kivutio kikubwa katika maonyesho hayo analitumia
katika shughuli zake za kila siku na lina uwezo wa kusafiri umbali wa
kilometa 180 kwa saa.
Mkurugenzi Ustawi wa Jamii,Maendeleo ya Wanawake, Vijana na
Wanawake kutoka Zanzibar Bw.Mohamed Salim Alli akifungua mdahalo wa
Vijana wakati wa Wiki ya Vijana katika Ukumbi wa VETA mkoani Iringa.
Vijana wakishiriki mdahalo wa wazi wa Wiki ya Vijana , Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere , Mbio za Mwenge wa Uhuru na Fursa za uwekezaji zinazopatikana katika mkoa wa Iringa leo katika ukumbi wa VETA Iringa.
Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.
Toa Maoni Yako:
0 comments: