Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Asangye Bangu akiongea na waandishi wa habari Wakati wa kutangaza kuanza kutumika kwa Huduma ya M-pesa kukusanyia marejesho ya mikopo kwa wanufaika wa bodi hiyo. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi Juma Chagonja.
---
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imetangaza kuanza kutumia huduma ya M-pesa katika kukusanyia marejesho ya mikopo kutoka kwa wanufaika hatua ikiwa ni katika mikakati ya bodi ya kuimarisha makusanyo ya urejeshaji wa mikopo hiyo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi Bw. Asangye Bangu amewaambia waandishi wa habari wakati wa zuinduzi wa huduma hiyo mpya jijini Dar es salaam kwamba bodi inaendela kujipanga kuhakikisha inaboresha njia za urejeshaji mikopo ili kuwpatia walengwa urahisi.

Amesema mojawapo ya kazi za Bodi ni kusimamia utoaji wa mikopo kwa wanafunzi waliodahiliwa kwenye vyuo vya elimu ya juu pamoja na urejeshwaji wa mikopo iliyotolewa na Serikali kwa waliokuwa wanafunzi wa elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 mpaka sasa kwa nia ya kuufanya mfuko wa Elimu ya Juu kuwa endelevu.

"Tunayofuraha kubwa sana leo kutangaza kwamba sasa wanufaika wa mikopo ya Bodi wanauwezo wa kutumia mfumo wa M-pesa kufanya marejesho ya mikopo yao moja kwa moja kwa Bodi."Alisema Bangu

Bingu amesema bodi inaimani kuwa M-pesa itawapatia urahisi wanufaika kuweza kutimiza wajibu wao kisheria wa kurudisha mikopo waliopatiwa kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu.

Amesema wanufaika wa mikopo wanapaswa kuanza kurejesha mikopo yao mara baada ya miezi 12 kuanzia wanapohitimu masomo ya elimu ya juu au wanapositisha masomo kwa sababu yoyote ile, akiwa ameajiriwa ama hajaajiriwa.

Bingu amesema wanufaika walioajiriwa wanalipa mikopo yao kupitia kwa waajiri wao ambapo hukatwa marejesho ya mikopo kwenye mishahara yao ya kila mwezi na mwajiri huwasilisha makato hayo kwenye Bodi kupitia kwenye akaunti zake huku wale ambao sio waajiriwa hupeleka huwasilisha marejesho ya mikopo katika benki za bodi.

"Wanufaika wanaorejesha mikopo yao kwa pesa taslim wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali wakati wa urejeshwaji wa mikopo yao kupitia kwenye akaunti za Benki ikiwa ni na benki hizo kutokuwa na matawi ya kutosha yaliyokaribu na warejeshaji wa mikopo pamoja na kutumia muda mwingi kwenye foleni."Alisema Bingu
"M-pesa itapunguza changamoto hizo na hatimae kuwajengea mazingira mazuri ya urejeshwaji wa mikopo, Bodi inatangaza rasmi kuanza kutumika kwa utaratibu huu mpya wa urejeshaji kwa M-pesa kuanzia sasa."
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: