Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akisimikwa kuwa Mshauri wa Watemi wa Kabila la wasukuma katika tamasha la Bulabo alilolizindua rasmi jana katika viwanja vya Kisesa wilaya ya Magu mkoani Mwanza likidhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti.


Mtemi Antonia akimkabidhi fimbo ya watemi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ikiwa ni ishara ya kuwa Mtemi
Mheshimiwa waziri mkuu akiwa sambamba na Mhasham Baba Askofu wa Jimbo la Mwanza Yuda Thadei Ruwaichi wakipiga ngoma kuashiria uzinduzi rasmi wa Bulabo 2013, huku wakishuhudiwa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo pamoja na Naibu wa Nishati na Madini Mh. Stephen Masele (aliyesimama nyuma ya waziri mkuu)
“Tutaendelea kutambua juhudi za Kanisa na Kituo cha bujora katika kudumisha mila na serikali itahakikisha inashirikiana na kituo hiki kuhakikisha tamaduni ,sana na mila zinadumishwa kwa ukanda wa ziwa Victoria “alisema Pinda.
'Ngoma imenoga lazima nijumuike'
Naibu waziri wa wizara ya Nishati na madini ambaye vilevile ni mbunge wa Shinyanga mjini Mh. Stephen Masele akisalimia wananchi waliofurika kwenye tamasha la Bulabo 2013.
Wake kwa waume na watoto wao wote wamekuja hapa.
Usikivu kusanyikoni..
Kundi la Makhilikhili toka mkoani Shinyanga likionyesha kazi.
Safu ya watemi na viongozi.
Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (kulia) akiwa na mwenyekiti wa zamani wa CCM mkoa wa Mwanza ambaye ni diwani wa Kisesa Mabina (katikati).
Waziri mkuu alisema kwamba Duniani kote urithi wa utamaduni umekuwa ukiathiriwa  na mabadiliko ya Kijamii, Uchumi na Siasa
ambayo ukosefu wa nia au kutaka uelewa na kuthamini mila na desturi za Jamii nyingine.
Wananchi waliofrika hapa uwanjani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: