Wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi na Taasisi zilizo chini ya Wizara wakiwa ndani ya Treni kuelekea katika kituo cha Buguruni Bahresa, ambapo waliadhimisha Wiki ya Mazingira Duniani kwa kufanya usafi katika eneo hilo leo asubuhi. Kauli Mbiu ya Wizara katika siku hii ni "Hifadhi maazingira kwa Uchukuzi Endelevu". Aidha Kauli mbiu ya Kitaifa ni 'Fikiri, kula; hifadhi Mazingira".
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania(TRL), Mhandisi Aman Kisamfu (wa pili kutoka kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), Dkt. Agnes Kijazi (wa tano kutoka kushoto) wakisubiria kuanza kazi ya Usafi katika eneo la Stehseni ya Buguruni Bahresa. Wizara ya Uchukuzi na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wamefanya usafi kwenye eneo hilo leo asubuhi ikiwa nisehemu ya maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani mbayo kitaifa inaadhimishwa Mkoani Rukwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi akifagia katika Stehseni yaBuguruni Bahresa, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Mazingira, leo asubuhi. Kilele cha wiki hiyo kitakuwa tarehe 5 Mwezi huu.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira na Usalama wa Usafiri Majini, Bi. Tumpe Mwaijande (aliyeshika mfuko) akifanya usafi katika eneo la Buguruni Bahresa kama ishara ya kuadhimisha Wiki ya Mazingira Duniani. Wafanyakazi wa wizara ya Uchukuzi pamoja na taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walifanya usafi katika eneo hilo kama ishara ya kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani ambapo Kauli mbiu ya Wizara hiyo ikiwa ni "Hifadhi Maazingira kwa Uchukuzi Endelevu".
Wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi na taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakifanya usafi katika Stesheni yaBuguruni Bahresa kama ishara ya kuadhimisha wiki ya Mazingira Duniani, Zoezi hilo la kufanya usafi limebeba kauli mbiu inayosema "Hifadhi Maazingira kwa Uchukuzi Endelevu".
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Uchukuzi)
Toa Maoni Yako:
0 comments: