Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, anapenda kuwaarifu Wataalamu wa Kada za Afya kuwa wamepangiwa vituo vya kazi kutokana na maombi ya kazi waliyowasilisha kwake kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

Watalamu wote wanatakiwa kuripoti katika vituo walivyopangiwa kabla ya tarehe 30 Juni, 2013. Baada ya muda huo kumalizika waajiri wanatakiwa kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili wale ambao  hawajaripoti nafasi zao ziweze kujazwa.

Aidha, Waajiri wote wanakumbushwa kukagua vyeti halisi (Original) vya kidato cha nne na kidato cha Sita pamoja na vyeti vya taaluma kabla ya kuwaajiri wataalamu hawa wa kada za afya.

Orodha ya majina ya Wataalamu waliopangiwa kazi na vituo walivyopangiwa inapatikana kwenye tovuti ya Wizara www.moh.go.tz Wizara haitatoa barua za kupangiwa vituo vya kazi kama ilivyokuwa hapo awali.

Nawapongeza kwa kupata nafasi hii ya kutumia utaalamu wenu katika kuwahudumia wananchi, na ninawatakieni kazi njema na utumishi uliotukuka.


20 Juni, 2013
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: