Mkurugenzi wa Heineken Tanzania, Uche Unigwe akiongea katika fainali za michuano ya mchezo wa Foosball ambapo uliwashindanisha timu ya Samaki Samaki na timu ya Liverpool ambapo Loverpool iliweza kuwashinda wenzao magoli 9-8.

Akiongea katika fainali hizo, Bw. Unigwe alisema bia ya kimataifa na maarufu Heineken ambao kwa mara ya kwanza ilianzisha mashindano ya mchezo wa foosball kwa kanda ya Afrika Mashariki ambapo jumla ya timu 280 ambayo walishiriki kutoka Dar es Salaam, Mwanza na Arusha. Kupitia Mashindano ya foosball, Heineken iliwapatia wateja wake uwezo wa kuijua ligi ya mabingwa.

Heineken iliwapa wateja wake changamoto yakuweza kuonyesha vipaji vyao kupitia mchezo wa foosball na waliweza pia kusherekea pamoja na marafiki.

Michuano hii imeona timu Champions na Timu Liverpool kutoka Tigo Tanzania na Samaki Samaki (kati kati ya mji) kutoka Dar es Salaam wakifika mwishoni wa njia mpaka finali ya michuano ya ligi mabingwa ambapo timu ya Liverpool iliweza kuwashinda wenzao magoli 9-8 katika mchuano mkali uliofanyika wakati wa Finali ya michuano iliyofanyika hoteli ya Golden Tulip Dar es Salaam na pia mechi ya UEFA ligi ya mabingwa ilionyeshwa live bila chenga na kuhudhuriwa na watu takriban 1,100 kutoka sehemu mbali mbali ya Dar.
 Waandishi wa Habari wakibadilishana mawazo huku wakiwa na furaha na bashasha, ni Tullo Chambo na mwanadada Aisha.
 Haka kabia ni katamu sanaaa...
Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi akiwa na mfanyakazi mwenzake, nao walikupo kushuhudia fainali hizo.
 Mazoezi ya kujinoa yakiendelea kabla ya mpira kuanza.
 ...Wandishi wa Habari wakibadilishana mawazo, hapa ni Victor akiwaelewa wenzake jambo.
Show love.
Tumependeza ehe!

Msanii maarufu wa kimataifa wa muziki wa kizazi kipya Cpwaa ambape aliteuliwa na kampuni ya bia Heineken Tanzania kusimamia michuano ya mpira wa mezani (Foosball) pamoja na kutangaza na kuhamasisha mchezo huo wakati wa mashindano ambayo ni endelevu ambapo mpango huo ulikamilishwa kati ya kampuni ya Brainstormmusic & Media Co. Ltd na Heineken Tanzania Limited. Akitangaza kuanza kwa fainali za michuano hiyo.
Msimamizi wa masuala ya mahusiano toka Heineken Tanzania, Nadine Kapya akionyeshwa jambo na mwanadada Sharon.
Moja moto moja baridi, wadau wakijipatia kinywaji laini cha Heinkene.

 Vijana wa Timu ya Samaki Samaki wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Heineken Tanzania, Uche Unigwe na
Meneja Biashara, Masoko wa Heineken Tanzania, Caroline Kakwezi.
 Wamiliki wa bar ya Samaki Samaki (kushoto) akiwa na Mmiliki wa Bar ya Trinity ambapo timu zao zilikuwa zikishindana.
 Vijana wa Timu ya Liverpool toka Tigo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Heineken Tanzania, Uche Unigwe na
Meneja Biashara, Masoko wa Heineken Tanzania, Caroline Kakwezi.
Meneja Biashara, Masoko wa Heineken Tanzania, Caroline Kakwezi (kushoto) akiongea na Meneja msimamizi wa matukio wa Heineken Tanzania, Moreen.
Mashabiki wa Timu ya Samaki Samaki.
Warembo toka Heineken Tanzania.

 Msanii maarufu wa kimataifa wa muziki wa kizazi kipya Cpwaa ambaye aliteuliwa na kampuni ya bia Heineken Tanzania kusimamia michuano ya mpira wa mezani (Foosball) akitoa kanuni za mchezo kabla ya mpambano.
 Mashabiki wa Timu ya Liverpool toka Tigo.
 Timu ya Samaki Samaki ikimenyena na Timu ya Liverpool.
 Wachezaji wa Timu ya Liverpol wakisangilia baada ya kushinda kipindi cha kwanza.
 Kipindi cha Pili kikiendelea...
Mashabiki wakifuatilia kwa makini.
 mchezaji wa Timu ya Liverpool akishangilia mara baada ya ushindi.
 nderemo na vifijo vilitawala.
Pongezi zikimiminika.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: