Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Diamond na Ney wa Mitego wakionyeshana mabavu.
Godzila stejin.
Msanii wa Kizazi Kipya, Mabeste akiwapa burudani wakazi wa Temeke katika tamasha Epiq Open Mi.
Msanii wa Kizazi Kipya, Madee akiwapa burudani wakazi wa Temeke katika tamasha Epiq Open Mi.
Marco Chali akielezea zoezi zima la Epiq Open Mic litakavyoendeshwa
Rama Dee na Mapacha jukwaani.
Mshindi wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012/2013 Walter Chilambo akiwaonyesha maufundi yake kwa wakazi wa Temeke na vitongoji vyake.
---
Katika kuelekea msimu wa sita wa shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search, kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imezindua Epiq Open Mic ikiwa ni nafasi nyingine kwa vijana wenye vipaji vya muziki kuonyesha vipaji vyao kabla usaili wa Epiq Bongo Star Serach haujaanza.
Epiq Open Mic inatarajiwa kuwapa nafasi vijana kujifunza misingi ya muziki kutoka kwa mmoja wa watayarishaji wa muziki maarufu zaidi nchini, Marco Chali.
Marco Chali ambaye pia ni mtunzi na mwimbaji, ametayarisha nyimbo nyngi ambazo zimeshinda tuzo ndani na nje ya nchi za wasanii kama Ms. Trinity kutokea Jamaica, A.Y wa Tanzania, Prezzo wa Kenya, J Martins kutoka Nigeria na wengine wengi.
Tamasha hilo la Epiq Open Mic, ambalo ni la bure lilizinduliwa rasmi kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Temeke tarehe 26 ya mwezi huu likisindikizwa na wakali kibao wa Bongo flavor kama Diamond Platnumz, Madee, Godzila, Ney wa Mitego, Mabeste na Mrap.
Akizungumza wakati wa kuzindua matamasha hayo, Afisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema kampuni ya Zantel inaaminini katika kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao.
‘Muziki ni ajira kwa vijana wengi, na kuamini hilo ndio maana kampuni ya Zantel imeamua kuwafikia vijana wote wenye vipaji na kuwapa nafasi ya kuonekana’ alisema Khan.
Baada ya uzinduzi wa tamasha la Epiq Open Mic Mwembe Yanga tamasha hilo litaendelea kila jumamosi kwenye makao makuu ya Zantel likiwapa nafasi vijana kujisajili na kurekod sauti zao.
Vijana watakaorekodi sauti zao watapigiwa simu na timu ya watayarishaji wa muziki chini ya Marco Chali pamoja na wanamuziki ili kuwapa ushauri wa namna ya kuboresha muziki wao zaidi.
‘Zantel imejipanga kutumia fursa hii kuwahamasisha vijana kushiriki katika kukuza vipaji vyao, kuongeza uelewa wa mambo ya muziki pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo katika muziki’ alisisitiza Khan.
Epiq Open Mic pia inatarajia kuwapa fursa ya kurekodi baadhi ya vijana watakaokua na vipaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments: