MGOMBEA Urais nchini Kenya, Uhuru Kenyatta, ameendelea kukalia kileleni katika matokeo yanayoendelea kutolewa kwa kupata 53% kutokana na kura zilizohezabiwa katika vituo zaidi ya 40%.

Matokeo hayo yaliyotangazwa masaa 7 yaliyopita, huku Raila Odinga, yeye akifuata kwa kujinyakulia 43%.

Hayo ni matokeo yanayoashiria kuwa mwelekeo wa Uchaguzi huo bado upepo upo kwa Kenyatta, anayechuana na mtu ambaye mwaka 2007 alikuwa juu mno akipendwa na Wakenya wengi na kusababisha kuundwa kwa serikali ya mseto kati yake na Mwai Kibaki.

Kura hizo zinahesabiwa kutoka vituo zaidi ya 40% huku mpaka sasa kura hizo zikihesabiwa kutoka zaidi ya nusu ya vituo vilivyoteuliwa kupigiwa kura katika Taifa la Kenya mwaka huu.

Mungu ibariki Kenya na uendelee kuwa Uchaguzi wa amani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: