Penzi Jipya ni kama Mkataba mpya wa
kazi.... Penzi jipya ni tamu, linakufanya ujisikie raha kama mtu aliyepewa
mkataba mnono wa ajira baada ya kutafuta kazi kwa msoto kwa muda
mrefu. Unapata mshawasha na kimuhemuhe huku mapigo yako ya mdukuo wa
moyo yakiwa juu ukidhani hali ile itakuwa hivyo milele lakini sivyo.
Kabla
hujaingia uhusiano mpya punguza munkari. Usiwe na pupa, soma mazingira
kwanza ili ujue kama utaweza kuhimili dhoruba za humo ndani.
Umejiandaaje
ukikuta Bosi wako, New partner, ni kimeo?... Kabla hujasaini mkataba wa
kazi, hata uwe mnono namna gani usome vizuri ili ujue kama vitu vyote
muhimu unavyohitaji kwenye mkataba vimeandikwa. Dont be in a rush!
Wengi
husaini mikataba ya Relationship kwa pupa kwasababu they are in need au
kuangalia hela tu, mwisho wa siku unakuta Mkataba haukupi Health
Insurance unaanza kujuta kwanini ulisaini... Sijui kama mmenielewa!
Imeletwa kwenu na Seth Giovanni,
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mapenzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: