Mshindi wa droo ya Ascend Y200 ya mwaka jana bw. Christian Evarist Mkama akiongea na waandishi wa habari Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kabla ya safari kuelekea nchini China.
Mshindi wa droo ya Ascend Y200 ya mwaka jana bw. Christian Evarist Mkama akiwa na mama mzazi bi. Eva Christian Amuko na mjomba wake bw. Fortunatus Christian Amuko, Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kabla ya safari kuelekea nchini China.
---
Kampuni ya simu ya mkononi ya Tigo Tanzania imempeleka bw. Christian Evarist Mkama nchini China ambaye ni mmoja kati ya washindi wawili wa droo ya kwanza ya Ascend Y200 ambayo ilifanyika mwaka jana tarehe 19 Desemba.

Kwa kuwa mshindi wa droo hii amejishindia tiketi ya bure ya kwenda na kurudi nchini China pamoja na kulipiwa gharama zote za safari, chakula na dola 200 kwa siku za matumizi.

Akiwa nchini China mshindi huyu atakaa siku nne na atatembezwa na kuonyeshwa sehemu mbalimbali za mji wa Guangzhou, na kupelekwa kwenye sehemu za utalii ya mlima Lotus.

Promosheni ya Ascend Y200 ilizinduliwa mwaka jana 2012 mwezi wa kumi (oktoba) kwa jumla kutakuwa na droo tano za Ascend Y200 na kila droo itakuwa na washindi wawili kwa jumla ya washindi kumi watapatikana kwenye droo hizi.

Kushiriki kwenye shindano hili mteja wa Tigo inambidi awe amenunua simu ya Ascend Y200 kwenye maduka ya Tigo yaliyosajiliwa na kujisajili kwenye kifurushi cha A-Smart package
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: