Makamu
mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Theophil Makunga pamoja na wakili wa
kujitegemea Juvenalis Ngowi wakimjulia hali Kibanda katika
taasisi ya mifupa (MOI).
Wakati mhariri mtendaji wa kampuni ya New Habari Corparation, Absalom Kibanda
akipelekwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi, chama cha
waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) kimeungana na waandishi
wa habari wote kulaani kitendo cha watu wasiojulikana kumvamia na
kumjeruhi vibaya Kibanda.
Kibanda
ambaye pia ni mwenyekiti wa jukwaa la wahariri, alikutwa na mkasa huo
usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Mbezi Beach jijini Dar es salaam
wakati akirejea kutoka kazini.
Kwa
mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa New Habari Corparation Hussein Bashe,
wavamizi hao ambao hawakuiba wala kupora kitu chochote, walimjeruhi
vibaya Kibanda sehemu za kichwani, huku pia wakimng'oa meno kadhaa,
kumkata kidole na kumchoma na kitu chenye ncha kali jicho lake la
kushoto.
Bashe alisema tukio hiyo ni la kusikitisha na halikupaswa kutokea kwani hakuna mwenye haki ya kumhukumu binadamu mwenzake.
Alisema
kuwa pamoja na jitihada za madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
bado wameshauriwa kumpeleka Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi zaidi
katika jicho lake ambalo linaonekana kupata athari zaidi kuliko sehemu
yeyote ya mwili wake.


Toa Maoni Yako:
0 comments: