Je asali inafaida gani kiafya?
Asali
hutumika sio tu kama chakula bali baadhi ya watu hutumia pia kama dawa.
Asali ina uwezo wa kuondoa chembe chembe haribifu mwilini na hivyo
kuulinda mwili dhidi ya maradhi mbali mbali.
Asali
ina virutubishi mbali mbali ikiwa ni pamoja na vitamin, madini na
protini kwa kiasi kidogo. Vile vile asali ina sukari nyingi ambayo ni
asilimia themanini(80%.
Kutokana
na asali kuwa na sukari nyingi, asali ina nishati-lishe nyingi kama
ilivyo sukari, hivyo ikitumika kwa wingi huongeza uzito wa mwili.
Asali
iliyokomaa kwa kawaida ina kiasi kidogocha maji, chini ya asilimia
ishirini (20%). Asali iliyoongezwa maji ina chacha mapema(inaharibika)
na inaota ukungu (fangasi), ambao wakati mwingine hauonekani kwa macho.
Kwa
kawaida asali iliyokomaa na isiyochanganywa majiikihifadhiwa vizuri
haiharibiki kwa miaka mingi, bila hata ya kuweka kwenye jokofu.
Kiasili,
asali ilikuwa ikitumika kwa sababu maalumuna kiasi kidogo tu, hivyo
hatari ya kumwongezea mtu uzito haikuwepo. Mara nyingi mtu anayetumia
asali alikuwa anatumia kijiko kimoja au viwili kwa siku na sio kila
siku.
Hata
hivyo, kumekuwa na imani potofu kwamba asali uweza kupunguza uzito wa
mwili na hivyo husababisha walengwa kutumia sasli kwa wingi, hii si
kweli .
Ikumbukwe
kwamba asali inanishati-lishe kwa wingi ambayo huchangia kuongeza uzito
wa mwili hivyo huweza kuleta madhara iwapo itatumika kupita kiasi.



Toa Maoni Yako:
0 comments: