Wajumbe wa Sekretarieti ya
CCM, wakiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akimpongeza
Dereva wa Treni aliyewafikisha Mjini Kigoma salama, Kambi Ali. Wengine pichani kutoka
kushoto ni Katibu wa Itikadi na Uenezi,
Nape Nnauye , Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Hajati Dk. Asha-Rose
Migiro na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela
Sekretarieti
ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imewasili salama mkoani Kigoma ikitokea jijini Dar
es Salaam kwa njia ya Reli.
Wakipokelewa
kwa Shangwe, takribani kila kituo njiani, Sekretarieti hiyo iliyoongozwa na
Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana pamoja na wajumbe wengine ambao ni Katibu wa
Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,
Hajati Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela uliwasili
Mjini Kigoma majira ya saa nne asubuhi na kupokelewa na Wakazi wa mji wa
kigoma.
Akizungumza
baada ya kuwasili Kigoma, Katibu Mkuu wa CCM, Kinana alisema yakuwa leongo la
safari yao hiyo ya Treni ni kuwadhihirishia wakazi wa Kigoma na taifa kwa
Ujumla kuwa Usafiri wa Treni ni wa uhakika na Serikali ya Chama cha Mapinduzi
kupitia Wizara ya Uchukuzi kuanzia sasa itasimamia kikamilifu usafiri huo na
kuboresha huduma maradufu na kuhakikisha safari zinaongezeka.
Nao baadhi
ya wakzi wa Mkoa wa Kigoma wameipongeza sana Sekretarieti hiyo kwa uamuzi wa
kusafiri kutoka jijini Dar es Salaam hadi Kigoma kuhudhuria maadhimisho ya
miaka 36 ya CCM kwa treni na kudai kuwa kufanya hivyo ni uzalendo tosha na
kuonesha haki kwa wananchi wote.
Katibu Mkuu akizungumza na wananchi wa Kigoma
Katibu wa Siasa na
Mahusiano ya Kimataifa, Hajati Dk. Asha-Rose Migiro akisalimia na wananchi wa
Kigoma
Wananchi wakisogea kuwapokea viongozi
Burudani hii ya ngoma ilikuwepo
Sekretarieti ikipokea heshima ktoka kwa Chipukizi.
Chipukizi wakimvisha Skafu Katibu Mkuu wakati wa mapokezi.
Katibu Mkuu akifurahia ngoma na Katibu wa Itikadina Siasa, Nape akipiga ngoma.
Kinana akizungumza na wanchi wa Kigoma
Wananchi wakiwa Stesheni kushuhudia viongozi hao. Picha na Mroki Mroki.
Toa Maoni Yako:
0 comments: