Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa
ufafanuzi kuhusu hoja mbalimbali zilizoibuliwa na jopo la APRM kuhusu
Demokrasia na Utawala Bora nchini Tanzania. Mhe. Rais alitoa ufafanuzi
huo mbele ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika
mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Mhe. Jacob Zuma, Rais wa Afrika Kusini na Mhe. Paul Kagame, Rais wa Rwanda nao walihudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU ambapo Tanzania iliwasilisha ripoti yake kuhusu Demokrasia na Utawala Bora.
Mhe.
Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea kutoa ufafanuzi kuhusu masuala ya
Demokrasia na Utawala Bora nchini Tanzania. Wengine katika picha ni
Waziri Bernard K. Membe (Mb) (wa pili kulia), Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, wakiwemo pia wajumbe na Wabunge waliofuatana
na Mhe. Rais Kikwete kuhudhuria Mkutano huo.
Mhe. Rais Kikwete (kushoto) akibadilishana mawazo na Mhe. Salum Barwany, Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini nje ya ukumbi wa mkutano nchini Ethiopia.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete katika picha ya
pamoja na ujumbe aliofuatana nao nchini Ethiopia ambao unajumuisha
Mawaziri, Wabunge na Timu ya APRM, Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments: