Ngowi akiwa na mwamuzi Jaap Van Niewenhuizen wa Afrika ya Kusini.
---
Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Matanzania Onesmo Ngowi atasimamia pambano la ubingwa wa dunia la vijana katika jiji la Johannesburg nchini Afrika ya Kusini.
Mpambano huo utawakutanisha mabondia Ilunga Makaba kutoka Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC) mwenye makazi yake nchini Afrika ya Kusini akipambana na bondia Gogita Gorgiladze anayetoka katika jiji la Tiblis, nchini Georgia. Georgia ilikuwa kati ya nchi zilizokuwa Umoja wa nchi za Kisoshalisti wa Sovieti (USSR).
Mabondia hao wenye wiwango vinavyolingana Georgita (12) na Makaba (12) watapambana kugombea mkanda wa vijana wa wa dunia (Youth Title) wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika uzito wa Cruiserweight tarehe 15 February, 2013.
Mpambano wa wawili hawa utafanyika katika hoteli ya nyota 5 ya Emperors Palace in Kempton Park, Gauteng katika jiji la Johannesburg, nchini South Africa.
Ngowi kama kamishna mkuu wa pambano hilo atasaidiwa na maofisa wafuatao: Refarii: Wally Snowball (Afrika Kusini). Jaji Namba moja:Simon Xamlashe (Afrika Kusini), Jaji namba mbili: Manuel Maritxalar (Spain) na Jaji namba tatu: Jaap Van Niewenhuizen (Afrika ya Kusini).
Mpambano huu ni kati ya mapambano zaidi ya 100 ya IBF yatakayofanyika katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati katika kipindi cha mwaka huu wa 2013 chini ya mradi wa IBF wa “Utali wa Michezo
Toa Maoni Yako:
0 comments: