Mwanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi Mkwajuni kata ya Kichangani Manispaa ya Morogoro, Christopher Mkude (8) akiwa na beseni lenye ndizi mbivu akiwa amebeba kichwani katika mtaa wa Juwata wakati akisaka wateja wa kuwauzia ndizo hizo ambazo alikuwa akiuza kati ya sh 100 hadi sh 150 ambapo alieleza kuwa fedha anazopata hununua vifaa vya shule.
Mkazi wa Manispaa ya Morogoro aliyejitambulisha kwa jina moja la Sengo akiwa amebeba madumu tupu ambayo hutumika kuhifadhia maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali wakati akisaka wateja wa kuwauzia katika eneo la Shan ambapo dumu moja huuzwa kwa sh 14,000 ikiwa ni bei ya awali mkoani hapa.
Kijana mkazi wa Manispaa ya Morogoro akikokota mkokote wenye kofia za aina mbalimbali wakati akipita katika barabara ya Madaraka eneo la Luna katika harakati za kusaka wateja wake kwa ajili ya kuwauzia kofia hizo mkoani hapa.
Mwanamke Manispaa ya Morogoro akiwa amebeba beseni lilijaa zambarau mara baada ya kuzinunua kutoka kwa vijana wanaochuma kwenye miti ya matunda hayo kisha kuwauzia wateja wake kwa bei ya rejareja ambapo kikombe chenye ujazo wa nusu lita huuza kiasi cha sh 200 mkoani hapa.
Kijana wa jamii ya kimasai kutoka mkoani Arusha akiwa amebeba viatu vya wazi zilivyotengenezwa kutokana na mazao ya mifugo akitembeza kusaka wateja wake katika mtaa wa Fondogolo Manispaa ya Morogoro ambapo pea moja huuzwa kati ya sh 15,000 hadi sh 18,000 ikiwa ni sehemu ya kujitafutia pesa kwa njia halali mkoani hapa.
Wafanyakazi wa kuoa takangumu katika kata ya Kingo wakisukuma mkokoteni uliosheheni viroba vya taka hizo mara baada ya kuzikusanya katika nyumba za kata hiyo wakati wakiendelea kutupa kwenye jaja ambapo nyumba moja hutozwa kiasi cha 1,500 kwa mwezi mkoani Morogoro
Vijana wakazi wa Manispaa ya Morogoro wakiteremsha madumu yenye maji kwa mmoja wa wateja wao kata ya Kihonda ambako sehemu kubwa ya maeneo la kata hiyo imekuwa na uhaba wa maji safi na salama kutokana na kukosa mfumo wa mamlaka ya majisafi (MOROWASA) ambapo dumu moja huuzwa kati ya sh 200 hadi sh 500 kulingana na umbali wa eneo mkoani Morogoro. Picha na Juma Mtanda, Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments: