Mheshimiwa Balozi, Peter Kallaghe, akipokea zawadi ya CD na DVD kutoka kwawanamuziki maarufu wa Kimataifa wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha na Mumewe Bwana Emmanuel Mbasha. Waimbaji hao wa nyimbo za injili hao wakiwa nchini Uingereza, walitembelea Miji ya Glasgow, Chemsford na Reading. 
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe, akiwa kwenye picha ya pamoja na wanamuziki maarufu wa Kimataifa wa nyimbo za Injili Flora Mbasha na Mumewe Bwana Emmanuel Mbasha (Kulia), Askofu Ernest Irungu, ambaye ni Kiongozi wa nyimbo za Injili na ni Mkuu wa Chuo cha Vision College of Theology kilichopo London, Uingereza, mama Zest Irungu (mke wa Askofu Irungu) na Bi. Mwambola, walipotembelea Ofisi za Ubalozi. Bw na Bi Mbasha wapo nchini Uingereza, wakitokea Amerika kujitangaza na kutangaza Injili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: