Kwa taarifa zilizopatikana kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari, zinasema kuwa msanii aliyekuwa akiugua kwa muda mrefu, mwigizaji mahiri Bongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amefariki dunia leo majira ya saa moja asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Marehemu Sajuki alikuwa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuwa amedondoka jiji Arusha mwishoni mwa mwaka uliopita ambapo alipokwenda kufanya shoo kuchangisha fedha kwa ajili ya kumpeleka tena India kupata matibabu..

Maandalizi ya msiba huo yatatangazwa baada ya wahusika na wadau kujipanga. Habari za kifo chake zimeanza kusambaa tangu saa moja asubuhi, hivyo wadau na mashabiki wake watapewa utaratibu juu ya msiba wa msanii huyo mwenye mafanikio katiika tasnia ya filamu Tanzania. milele,” alisema.

Kifo cha Sajuki kwa wasanii kimefungua dimba kwa mwaka 2013, huku ukiwa na kumbukumbu za kuondokewa na wasanii watano katika kipindi cha mwaka 2012, akiwamo Steven Kanumba, Sharomillionea na wengineo.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

8 comments:

  1. Inna lilahi wainaillay rajiun.

    ReplyDelete
  2. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU SAJUKI MAHALI PEMA PEPONI,jamani ndg watanzania wenzangu sajuki kaimaliza zamu yake aliyotumwa na mwenyezi mungu kilichobaki tijiulize mimi na wewe tumejiandaa vipi,bwana alitoa bwana ametoa.jana la bwn lihimidiwe.AMEN.

    ReplyDelete
  3. Mungu amulaze panapo msitahil

    ReplyDelete
  4. Mungu amulaze panapo msitahili

    ReplyDelete
  5. Mungu amulaze panapo msitahili

    ReplyDelete
  6. Mungu jamani twaomba atuepushie mbali na maradhi

    ReplyDelete