Juma Nature akiwapagawisha mashabiki.
Mkongwe Profesa J akiwapelekesha puta mashabiki.
Stamina akionyesha anavyotawala jukwaa.
Linex akiwapagawisha mashabiki.
Mkongwe Luteni Kalama wa Gangwe Mob akifanya vitu vyake.
Inspekta Haroun akikamua.
Wanamuziki wa Twanga pepeta wakiwajibika jukwaani.
KR ‘Mulla’ akifanya vitu vyake.
Inspekta Haroun akiwa na mkewe jukwaani.
Umati wa mashabiki ukiserebuka.
Stamina akikamua.

 
Juma Nature akiserebuka.
Linex akiwapa hi mashabiki wake.
Profesa J akiwa na Linex katika picha ya pamoja.
Prefesa J akizidi kuwapa raha mashabiki.
Luteni Kalama akiwa na shemeji yake.
Kundi zima la Gangwe Mob likiwapagawisha mashabiki.
 
Juma Nature akiwaimbisha mashabiki.
---
USIKU wa kuadhimisha kuanza kwa Mwaka Mpya wa 2013 ulishuhudia burudani ya kukata na shoka katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live ulioko Mbagala, ambapo wasanii kadhaa wa muziki wa kizazi kipya walitoa burudani ya kufa mtu.
Wasanii ambao waliwafanya mashabiki wasitulie katika viti vyao ni wakongwe Profesa J, Inspekta, Juma Nature, pamoja na wasanii wanaokuja juu katika fani hiyo ambao ni Linex na Stamina, huku bendi ya African Star ‘Twanga Pepeta’ wakiwapindisha migongo mashabiki.
(PICHA ZOTE: ISSA MNALLY NA RICHARD BUKOS / GPL)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: