Mkurugenzi wa Women in Balance Dina Marios akizungumza na wageni waalikwa kufafanua hatua ya awali ya maandalizi ya kufanyika kwa tukio la mafunzo ya‘Kitchen Party Gala’ kwa kina mama jinsi ya kuishi ndani ya ndoa ili kujenga familia bora litakalofanyika mnamo tarehe 21 mwezi huu.

Akifafanua zaidi amesema tukio hilo la 4 litakalokuwa la mwisho kwa mwaka huu litakalofanyika kuanzia saa 8 mchana mpaka saa 4 usiku litafanyika katika hali ya ubora zaidi katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Aidha amewataka wanawake kuhudhuria kwa wingi ili waweze kupata faida kwa ajili yao binafsi na kuweza kuwa waalimu bora kwa waume zao jambo litakalosaidia kuepusha migogoro ya mara kwa mara inayopelekea kuvunjia kwa ndoa.

Wadhamini wa Kitchen Party Gala ni TSN Super Market, Sossi, Coca Cola na Clouds Fm.

Mahali:Diamond Jubilee VIP hall
Muda:Kuanzia saa nane mchana mpaka saa nne usiku.
Kiingilio ni Tsh 30,000. Ukitaka kubook meza ya watu kumi piga namba 0787583132, 0716485666

Safarii hii ukiacha wasemaji kuna burudani ya kila aina ukizingatia ni ya mwisho kabisa kwa mwaka huu.Bila kusahau chakula,na vinywaji laini.
 
RANGI YA SIKU.
Kwa muda kina dada/mama mmekuwa mkitoa maoni mnataka kushona nguo mtokelezee. Basi rangi ya siku ni rangi ya chenza (tangerine tango)color of the year 2012.

Ishone utakavyotaka wewe iwe kitambaa cha kawaida, kitenge, kanga, batiki, au ukachanganya vyovyote ili mradi uzingatie rangi ya siku.
Mmoja wa wadhamini wa Women in Balance Kitchen Part Gala Mwakilishi kutoka TSN Super Market Lizbeth akijitambulisha kwa wageni waalikwa na kuelezea lengo lao ya kudhamini event hiyo ambao wanaamini wanawake wakiwezeshwa wanaweza kwasababu ya mifano mingi imeonekana katika Bunge na Serikali kwa Ujumla.
Meneja Msaidizi wa Mauzo na Huduma kwa Wateja Wa Shekinah Garden Bi. Violeth Lussagana akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wake ambapo amesema wao kama wadhamini wameamua kuunga mkono shughuli hiyo kwa sababu ‘products zao’ zinafiti sana wanawake, kwa sababu wanawake wao ndio kila kitu kuanzia katika sherehe kwa mfano katika kutafuta mapambo, maandalizi ya sherehe na wanaamini kuwa wanawake wanaweza kufanya chochote iwapo watapewa nafasi.
Ameongezakuwa bustani nzuri ya Shekinah Garden iliyoko karibu na Samaki Samaki Mbezi Beach ilipofanyikia hatua ya awali ya maandalizi ya kufanyika kwa Women in Balance ‘Kitchen Party Gala’ imetengenezwa na mwanamke, ikiwa ni ishara kuwa ukimwezesha mwanamke, umeiwezesha jamii nzima.
Na huu ndio muonekano wa Shekinah Garden iliyopo karibu kabisa na Samaki Samaki Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Mwanasaikolojia Aunty Sadaka Ghandhi naye atakuwa ni mmoja wa watoa mada katika 'Women in Balance Kitchen Party Gala' ambapo amewataka kina mama na binti zao wajitokeze kwa wingi kujumuika pamoja katika siku hiyo muhimu ya tarehe 21 mwezi huu.
Mwalimu wa Saikolojia wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Criss Mauki akizungumza kama mmoja wa watakaokuwa wazungumzaji katika Women in Balance ‘Kitchen Party Gala’ hiyo na kufafanua umuhimu wa watu kuelewa dhana ya mahusiano kwa watu wa aina zote wakiwemo walioko katika mahusiano, walioachana na wanaokutana katika mazingira tofauti.
Barbara Hassan wa Powerbreak Fast (katikati) na Asmah Makau wa Clouds Radio katika pozi.
Mkurugenzi wa Women in Balance Kitchen Party Gala Dina Marios (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na marafiki waliohidhuria Pre-Event ya Women in Balance Kitchen Party Gala iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Sehemu tulivu yenye upepo wa asili Shekinah Garden iliyopo karibu na Samaki Samaki Mbezi Beach.
Shekinah Garden iliandaa chakula kwa wageni waliohudhuria Pre-Event ya Women in Balance Kitchen Party Gala.
Pichani Juu na Chini ni Mkurugenzi Women in Balance Dina Marios katika picha za kumbukumbu na wageni waalikwa.
Warembo waliohudhuria Pre Event ya Women in Balance Kitchen Party Gala.
Dina Marios na wageni waalikwa. Kauli mbiu ni "MWANAMKE KUWA MFANO".
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: