Meneja wa Bia ya Safari Lager, Kabula Nshimo (kushoto) akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu washindi bora 6 waliofuzu katika shindano la
shabiki bomba wa Superfans Dar es Salaam
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Kabula Nshimo akiwa na baadhi ya washindi wakiwa na t-shirt za Castle Lager
Mmoja wa walioingia sita bora kutoka Iringa, Denis Mlowe
John Mosha kutoka Dar es Salaam
Yahya Hamza kutoka Mwanza
Filberth Nestory kutoka Dar es Salaam.
Steven Chuma kutoka Dar es Salaam
---
Na Mwandishi Wetu.
HATIMAYE mashabiki sita
wakaochuana ili kupata wawili kupitia shindano la kusaka mashabiki bora wa Ligi
Kuu ya England, maarufu zaidi kwa jina la ‘Castle Lager Superfans’,
wamejulikana.
Washindi hao sita
wamepatikana kutokana na mchujo mkali kutoka kwa mashabiki 361 waliojitokeza
kushiriki shindano hilo linaloendeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
kupitia kinywaji chake cha Castle Lager.
Akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Bia ya Castle Lager, Kabula
Nshimo alisema ilikuwa ni mchujo mgumu, kutokana na wingi wa mashabiki
waliojitokeza.
Kabula alisema, miongoni
mwa hao sita, watapatikana wawili ambao ndio watakaoungana na mashabiki kutoka
nchi nyingine kuunda timu ya ushangiliaji katika fainali za Kombe la Mataifa
Afrika, zitakazofanyika Afrika Kusini mwakani.
Aliwataja mashabiki hao
sita na mikoa wanayotoka ikiwa kwenye mabano kuwa ni, Stephen Chuma , John
Mosha, Filbert Nestory (Dar es Salaam), Charles Mbaza (Arusha), Denis Mlowe
(Iringa) na Yahaya Hamza (Mwanza).
Castle Lager ambao pia ni
wadhamini wenza wa Ligi Kuu ya England, itawatembeza mashabiki hao mikoa yote
ili kuomba kura, pia kupitia promosheni mbalimbali zitakazoendeshwa nchi nzima.
Kabula alisema, mashabiki
361 walijitokeza kwa kutuma picha zao katika mtandao wa kijamii wa Facebook na
promosheni walizoziendesha katika mikoa mbalimbali.
Meneja huyo alisema, baada
ya mchujo walipatikana washindi 32 kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Iringa,
Shinyanga, Mwanza, Arusha na Kilimanjaro, ambao walipigiwa kura na kupatikana
15.
“Katika hao 15 ndio ambao
walifanyiwa mahojiano ya ana kwa ana, hivyo wamechujwa na kupatikana sita,
ambapo watasakwa washindi wawili ili waunde timu ya Castle Lager Superfans
Tanzania,” alisema.
Kabula alisema washindi
hao wawili watakaopatikana, wataungana na wengine kutoka Swaziland, Zambia,
Afrika Kusini na Zimbabwe ili kuunda timu ya ushangiliaji itakayogharamiwa kila
kitu katika fainali za Kombe la Mataifa Afrika hapo mwakani. Fainali hizo
zitafanyika Afrika Kusini.
Mashabiki hao sita unaweza
kuwapigia kura kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno ukitaja jina la mshiriki
kwenda namba 0683 536631.
Toa Maoni Yako:
0 comments: