Balozi wa Airtel nchini Ambwene Yessaya (AY) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chekechea ya shule ya msingi Buguruni Viziwi walipotembelea shule hiyo mwishoni mwa wiki hii.Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA wanaendesha mradi maalum utakaowezesha wanafunzi hao wenye uhitaji maalum kupata vifaa vya kujifunzia.
Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi akiangalia ujuzi wa wanafunzi wa shule ya Buguruni viziwa alipotembelea shule hiyo mwishoni mwa wiki hii. wakati AIRTEL na Balozi wao msanii AY walipofanya ziara maalum ya kuhamasisha jamii kuchangia wanafunzi hao wa shule ya msingi Buguruni viziwi kupata vifaa vya kujifunzia kwa kushirikiana na BAMVITA. Mwalimu wa shule ya msingi Buguruni Viziwi akiwapa ujumbe wanafunzi wa shule hiyo baada ya kutembelewa na wafanyakazi wa Airtel, kutoka kushoto ni mwamlimu mkuu wa shule hiyo bi Winfrid Jeromia, akifuatiwa na Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi na Airtel Ambassador Ambwene Yessaya (AY). Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA wanaendesha mradi maalum utakaowezesha wanafunzi hao wenye uhitaji maalum kupata vifaa vya kujifunzia Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi akiongea na wanafunzi wa shule ya Buguruni Viziwi mwishoni mwa wiki hii wakati ambapo airtel walitembelea shule ya msingi viziwi kuhamasisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia pamoja na nyenzo mbalimbali kupitia mradi maalumu wa kuchangia vitabu unaoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA, kushoto ni Mwalimu wa shule hiyo bi Judith Kaneno akifuatiwa na Airtel Ambassador ajulikanae kwa jina la AY( Ambwene Yessaya) kulia ni Mwalimu mkuu bi. Winfrid Jeromia.
---
Wanafunzi Buguruni Viziwi na Balozi wa Airtel AY-waomba Watanzania kuchangia vifaa vya kufundishia.
Ni moja kati ya shule zitakazofaidika na mradi wa Airtel na BAMVITA
Wanafunzi wa shule ya Buruguni viziwi wameomba watanzania na wadau mbalimbali kuchangia ili kufanikisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia pamoja na nyenzo mbalimbali kupitia mradi maalumu wa kuchangia vitabu unaoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA. Wanafunzi hao waliosema hayo wakati Airtel pamoja na balozi wake AY walipotembelea shuleni hapo mwisho mwa wiki hii.
Wanafunzi wa shule ya buruguni viziwi
ambao mbali na masomo ya darasani pia wanafundishwa kazi za stadi,
walionekana kufanya kazi za stadi za mikono ikiwemo kutengeneza shanga
pamoja na mazulia madogo ya miguu, wametia hamasa na kuthibithisha
kwamba wakiwezeshwa na kupatiwa nyenzo wanauwezo mkubwa sana wa kufanya
shughuli za stadi na ubunifu.
Akiongea katika ziara hiyo Meneja
huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi alisema “leo tumetembelea shuleni
hapa ikiwa ni mwendelezo wa utaratibu wetu katika kubainisha mahitaji ya
ziada ambazo shule hizi zenye mahitaji maalumu zinahitaji. Shule ya
Buruguni viziwi ni moja kati ya shule zitakazofaidika Mradi huu
unaoshirikisha Airtel na BAMVITA una lengo la kusaidia kuendeleza
kiwango cha Elimu hapa nchini na kutoa nafasi kwa jamii yetu kuweza
kushiriki na kuchangi elimu ya msingi kwa watoto wenye mahitaji maalum. ‘
Naye Balozi wa Airtel AY Ambwene
Yesaya alisema “ Tunawashukuru watanzania kwa kuitikia wito na kuanza
kuchanga na tunaendelea kutoa wito kwa watanzania kuendelea kuchangia
kwa kutuma neno “Vitabu” kwenda namba 15626 na kwakufanya hivyo kila SMS
utakayotuma utakuwa umechangia shilingi 200 au kuchangi kiwango
chochote kupitia Airtel money 0788 041361 ambapo jina la fumbo ni
VITABU.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi
Buguruni Viziwi bi. Winfrid Jeromia alikuwa na haya ya
kusema”tunaishukuru sana Airtel kwa kuweza kuja na mradi kama huu wa
kuweza kuinua Elimu hapa nchini na kurahisha mazingira yetu ya
ufundishaji hapa shuleni. Tunawaomba watanzania wengine na makampuni
mengine makubwa yajitokeze kwa wingi kuweza kuchangia katika mradi huu
ili kuinua wigo wa Elimu hapa nchini.
Kampeni hii ya kuchangia vifaa kwa
shule zenye mahitaji maalumu inayoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana
ilizinduliwa Agosti 23 2012 na itaendelea kwa muda kwa mienzi mitatu.
Kwa kuanzia shule tatu za jijini Dar es Salaam ambazo ni Uhuru
Mchanganyiko, Sinza Maalum, na Buguruni Viziwi zitafaidiaka na mradi
huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: